Tuesday , February 21 2017

Recent Posts

Wakazi wa kisiwa cha Kojani Pemba wahamasika kuchimba vyoo na kuvitumia baada ya kupatiwa elimu ya afya na usafi wa mazingira.

kojani

Na Masanja Mabula -PEMBA WAKAAZI wa kisiwa cha kojani wamesema  juhudi zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi mbali mbali juu ya kuwaelimisha umuhimu wa matumizi ya vyoo  zimeleta mafanikio ambapo kwa sasa wamehamasika kuchimba vyoo na kuvitumia. Wamesema kabla ya kuelimishwa umuhimu wa kutumia vyoo, walikuwa wakitumia sehemu za fukwe …

Read More »

HUSSEIN MACHOZI KUVUNJA UKIMYA NA ‘NIPE SIKUACHI’ CHINI YA COMBINATION SOUND

macho

Baada ya kukaa kimya kwa miezi mingi bila kuachia wimbo, Hussein Machozi anatarajia kuachia wimbo mpya wiki chache zijazo. Wimbo huo unajulikana kwa jina la ‘Nipe Sikuachi.’ Wimbo huo umetayarishwa na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa Bongo Flava katika miaka tofauti, Man Walter kupitia studio zake za Combination …

Read More »

Katibu Sekretarieti ya kupambana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu awapa somo wapelelezi polisi, mahakimu, waendesha mashtaka nchini

mwag1

Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, akitoa hotuba ya kufunga Mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Wizara hiyo ambapo …

Read More »

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TAWLA CHAKUTANA NA MADIWANI WA WILAYA TATU ZA JIJI LA DAR ES SALAAM

1

Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile akizungumza na Waganga Wakuu wa Wilaya, Maafisa Maendeleo wa Jamii, Wanasheria, Madiwani na Maafisa Mipango wa Halmashauri/Wilaya kutoka  Wilaya  tatu za Mkoa wa Dar Es Salaam Kinondoni Ilala na Temeke  pamoja na Waandishi wa  habari waliopata fursa ya kushiriki wakati akifungua semina ya kupata …

Read More »

FAO YATOA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 280 KATIKA MCHAKATO WA KUPITIA UPYA SERA YA TAIFA YA MISITU YA MWAKA 1998

2

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence  Milanzi ( kushoto)  akizungumza kabla kutia saini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika  la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)  ya  kupitia upya   Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo  imekuwa …

Read More »

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE YAWAAGA WAFANYAKAZI WAKE WANAOHAMIA HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA NA CHUO KIKUU CHA TIBA NA SAYANSI SHIRIKISHI (MUHAS) KAMPASI YA MLOGANZILA

09

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi wanne wa Taasisi hiyo ambapo watatu kati yao wanahamia  Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma na mmoja anahamia Hospitali ya …

Read More »

MABADILIKO MADOGO NA NYONGEZA YA WAJUMBE KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE

Capture

Spika  wa  Bunge  Mhe.  Job  Ndugai  (Mb)  amefanya  nyongeza  na  mabadiliko  ya  baadhi  ya  Wajumbe  katika  Kamati  za  Kudumu  za  Bunge ili kuwawezesha Wabunge wapya kuwa  Wajumbe  katika  Kamati  za  Kudumu  za  Bunge ikiwa ni pamoja  na  kuziwezesha  Kamati   kutekeleza  majukumu  yake  kwa  ufanisi  kutoka  na  uwiano wa  Wajumbe  katika  Kamati  hizo.  Wabunge  wapya  waliopangiwa   Kamati  za  Kudumu  za  Bunge  ni  pamoja  na; (a)  Mhe.   Abdallah   M.   Bulembo   (Mb)  amepangiwa  kuwa  Mjumbe  wa  Kamati  ya          Kudumu ya   Bunge  ya  Bajeti; (b)   Mhe.  Anne  K.  Malecela  (Mb) amepangiwa  kuwa  Mjumbe  wa  Kamati  ya  Kudumu          ya  Bunge  ya  Nishati  na  Madini;   amepangiwa  kuwa  Mjumbe  wa  Kamati  ya  Kudumu ya  Bunge  ya  Huduma  na  Maendeleo  ya  Jamii;  na (d) Mhe.  Prof.  Palamagamba  P.A  Kabudi  (Mb) amepangiwa  kuwa  Mjumbe  wa  Kamati          ya  Kudumu  ya  Bunge  ya  Katiba  na    Sheria. Aidha, pamoja  na  nyongeza  hiyo  ya  Wajumbe  kwenye  Kamati  za  Bunge, Mhe  Spika  pia  amemuamisha  Mhe.  Pudenciana  W.  Kikwembe  (Mb)  kutoka  katika  Kamati  ya  Kudumu  ya  Bunge  ya  Utawala  na  Serikali  za  Mitaa na  kuwa   Mjumbe  wa  Kamati  ya   Kudumu  ya   Bunge  ya  Miundombinu. Mabadiliko  haya  yamefanywa  chini  ya  Kanuni  ya  116  (3)  hadi (5)  ya  Kanuni  za  Kudumu    za  Bunge,  Toleo  la  Januari,  2016  inayompa  Spika  Mamlaka  ya  kuteua  Wabunge  ili wawe  Wajumbe  katika Kamati mbalimbali za Bunge ikiwa ni pamoja na Mamlaka  ya  kuongeza,  kubadilisha  au  hata  kupunguza  idadi  ya  Wajumbe  katika  Kamati  za  Kudumu  za  Bunge. Kwa   mujibu   wa   waraka   Na.  01/2017  uliotolewa   na  Mhe   Spika,  mabadiliko   haya   ya  wajumbe  kama  ilivyoainishwa  hapo  juu  yataanza  kutekelezwa  mara  moja  kuanzia  mwezi   huu wa Febuari,  2017. Imetolewa na: Kitengo  cha  Habari,  Elimu  na  Mawasiliano  Ofisi  ya  Bunge  DODOMA 20  Febuari,  2017 

Read More »

SWALEHE -S/M NIANJEMA YAKABILIWA NA UHABA WA MADAWATI NA MADARASA

nia2

Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Nianjema, Bagamoyo ,Ally Swalehe akizungumzia changamoto zilizopo shuleni hapo ikiwemo uhaba wa madawati . (picha na Mwamvua Mwinyi) Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Nianjema, Bagamoyo wakiwa wameketi kwenye madawati yaliyotolewa msaada kutoka kwa mkurugenzi wa shule za Feza kwa kushirikiana na …

Read More »

RT yakamilisha maandalizi hatua ya kwanza Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika ‘World Cross Country’

besu

  SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limekamilisha hatua ya kwanza na ya muhimu ya maandalizi ya kuelekea Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika ‘World Cross Country’ zitakazofanyika Kampala Uganda Machi 26, Mwaka huu.   Jumamosi, Februari 18 RT iliendesha Mashindano ya Taifa ya Mbio za Nyika katika Viwanja vya …

Read More »

AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA WAJASILIAMALI WANAWAKE WA MKOA WA DAR ES SALAAM YALIO CHINI YA TAASISI YA MANJANO YAENDELEA

kinna

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha ofisini kwake, Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, baada ya kufika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo, leo Feb 20, 2017.   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuonyesha sehemu ya kuketi, Balozi …

Read More »

HIFADHI YA TAIFA YA VISIWA VYA RUBONDO YANG’ARA ONGEZEKO LA WATALII

nde2

MNYAMA AITWAYE NZOHE ANAYEPATIKANA KATIKA HIFADHI YA RUBONDO TU TANZANIA NZIMA MWENYE RANGI NYEKUNDU/BROWN  NI DUME NA RANGI YA JIVU NI JIKE NA MWISHO PICHA YA NDEGE WALIOPO RUBONDO. ……………………………………………………………… Judith Mhina- Habari MAELEZO Idadi ya watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Visiwa cha Rubondo imeongezeka kutoka watalii 452 kwa …

Read More »

ZAIDI YA WANANCHI 500 WAPIMA AFYA BONANZA LA WANAHABARI

MUNGI

Mkuu wa Mawasiliano  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Bw. Innocent Mungy akizungumza katika bonanza hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. ……………………………………………………………………. Na Hassan Silayo Zaidi ya wananchi 500 wakiwemo waandishi wa Habari na Maafisa Mawasiliano Serikalini wamepima afya katika bonanza lililoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano serikalini, jukwaa la wahariri na …

Read More »

“Tunatamani ifike mahali watanzania wakiweke kiswahili kwenye roho zao” Prof. Ole Gabrieli

images

Immaculate Makilika- MAELEZO Serikali imesema inatamani kuona watanzania wanakiweka  kiswahili kwenye roho zao kwa kufikiri na kuzungumza lugha hiyo katika maeneo na shughuli mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili kukienzi pamoja na kuipa heshima inayostahili. Akizungumza katika kipindi cha Je tutafika?  kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Channel ten,  Katibu …

Read More »