Thursday , April 27 2017

Home / BURUDANI / SERA YA FILAMU KUWAKOMBOA WASANII WA FILAMU NCHINI TANZANIA.

SERA YA FILAMU KUWAKOMBOA WASANII WA FILAMU NCHINI TANZANIA.

Katibu Mtendaji, Bodi ya Filamu nchini Tanzania, Mama Joyce Fissoo.
Na BMGHabari
Bodi ya Filamu nchini imebainisha kwamba kukamilika kwa sera ya kusimamia uendeshaji wa tasnia ya filamu, kutasaidia kuwakomboa wanatasnia hiyo kwa kuinua kuinua uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.
 
Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo, Bi.Joyce Fisso, aliyasema hayo jana wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Break Fast On Saturday kinachoendeshwa na watangazaji Philip Mwihava na Godfrey Kusolwa.
 
“Kuwa na sera ya filamu pia kutaongeza wigo wa uwekezaji kwenye tasnia hii, kutasaidia kuondoa baadhi ya changamoto kwani bado taasisi za kifedha hazitambui sekta hii ikizingatia kwamba mswada wa filamu ni kama mtaji hivyo lazima sera iweze kutanabaisha wazi ili kuwasaidia wanatasnia kupata mikopo kwa njia rahisi kupitia miswada”. Amesema Fissoo.
 
Fissoo amesema sera ya filamu itasaidia kuwezesha muono kwamba tasnia ya filamu ni ajira, ni uchumi na inatoa fursa za kimaendeleo kwa wadau wake ambapo bodi ya filamu inaendelea kupokea maoni ni namna gani sera hiyo iwe.
Pia Bi.Fissoo aliwahamasisha watanzania kuzipigia kura filamu za Tanzania ili zishinde tuzo za Africa Magic Viewer Choice za nchini Nigeria, akisema “Filamu hizo
ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming ambazo zinawania tuzo za filamu bora na
Siri ya Mtungi ambayo inagombea filamu bora ya lugha ya Kiswahili. Niwaase
Wanzania, ushindi wa filamu hizi ni sisi kuwapigia kura hawa vijana wetu ambao
wameshika bendera yetu kwenda kutuwakilisha kule Nigeria, niwasihi waweze
kuzipigia kura na wahakikishe wanahamasisha marafiki zao pia kuzipigia kura ili
nafasi zote tuzo zije Tanzania”.
Mtayarishaji wa filamu nchini, Staphord Kihole (pichani) ambaye pia alikuwa kwenye kipindi hicho, ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kuzipigia kura filamu za kitanzania ili zishinde tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards zinazofanyika nchini Nigeria ikiwemo filamu yake ya “Naomba Niseme” inayowania vipengele viwili, kikiwemo kipendele cha Best East Africa na Best All Africa kinachoamuliwa na majaji.
 
Ili kuzipigia kura filamu za Tanzania ambazo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming, unapakua Application ya We Chat, unajisajiri kwenye Africa Magic kwa kutumia nambari ya simu na kisha unatafuta kipengele cha AMVCA na utaweza kupiga kura kadri upendavyo ambapo mtu mmoja anaweza kupiga kura hadi 100 kwenye filamu tofauti tofauti.
 

About bukuku

Check Also

A

Waibuka Washindi Kampeni Ya ‘Hamasika Na Masika’ Ya Mobisol

Mwakilishi wa Mobisol mkoa wa Dar es Salaam,Allan Rwechungura (kulia) akiwasiliana na mmoja wa washindi,kushoto ni …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *