Thursday , June 22 2017

Home / MICHEZO / UKWELI WA USAJILI WA NIYONZIMA KUSAINI SIMBA MIAKA MIWILI UPO HAPA

UKWELI WA USAJILI WA NIYONZIMA KUSAINI SIMBA MIAKA MIWILI UPO HAPA

Niyonzima

Baada ya Yanga kumsajisili Ibrahim Ajibu kwa dau nono la shilingi milioni 50 pamoja na kumpa usajifiri wa gari, sasa Simba nao wamejibu mapigo.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa mazungumzo baina ya kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima na Simba yamefikia pazuri.

Niyonzima ambaye amemaliza mkataba wa kuitumikia Yanga hivi karibuni pia alikuwa katika mzungumzo ya kusaini mkataba mpya kuendelea kuichezea Yanga lakini hawakuwa wamefikia kwenye hatua nzuri.

Mtu wa karibu wa Simba ametoa tamko hili baada ya kuulizwa juu ya tetesi hizo: “Ni kweli kaka Niyonzima amesaini Simba miaka miwili kwa dau nono.”

Pamoja na hivyo, rafiki wa karibu wa Niyonzima alipoulizwa juu ya suala hilo, amesema: “Siyo kweli bado hajasaini Simba ila ni kweli alizungumza nao jana.”

About Alex

Check Also

_93630299_rexfeaturesd

TETESI ZA SOKA ZA USAJILI BARANI ULAYA ALHAMISI JUNI 22,2017

 Na Salim Kikeke Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, atakaidi hatua ya Antonio Conte na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *