Saturday , October 21 2017

Home / MCHANGANYIKO / MSANII DAVIDO KUHOJIWA NA POLISI NCHINI NIGERIA KUFUATIA KIFO CHA RAFIKI YAKE

MSANII DAVIDO KUHOJIWA NA POLISI NCHINI NIGERIA KUFUATIA KIFO CHA RAFIKI YAKE

_98282433_e299b449-9b12-4085-a36c-771b90832e90

Polisi katika mji wa Lagos nchini Nigeria wanasema kuwa wanamchunguzua mwanamuziki Davido, ambaye jina lake kamili ni David Adeleke, kufuatia utata unaozunguka kifo cha rafiki yake Tagbo Umeike.

Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa Davido hachukuliwa kuwa mshukiwa wakati huu, lakini akathibitisha kuwa mwanamuziki huyo wa afrobeats, aliitwa kuhojiwa pamoja na familia ya Tagbo, ambao walikuwepo wakati wa kifo chake.

Tunachunguza ni wapi Davido alienda, kanda ya video, ili kupata picha wazi kuhusu kile kilichotokea. alisema msemaji huyo.

Bw. Tagbo, rafiki yake Davido alifariki tarehe 3 Oktoba na mwili wake ukaachwa nje ya hospitali mjini Lagos.

Davido amekana kabisa kuhusika kwenye kifo cha rafiki yake.

CHANZO:BBCSWAHILI

About Alex

Check Also

PIX 2

Dkt. Ndungulile : Tujitokeze Kupima Afya Mara kwa Mara.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndungulile …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *