Saturday , October 21 2017

Home / MCHANGANYIKO / MKE WA RAIS MAGUFULI ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WATOTO YATIMA ZANZIBAR

MKE WA RAIS MAGUFULI ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WATOTO YATIMA ZANZIBAR

DSC_1211

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli kushoto akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein mara baada ya kuwasili katika nyumba ya kulelea Watoto Mazizini kwa ajili ya kusalimiana nao na kuwapa msaada wa Chakula ikiwa ni miongoni mwa Ziara yake  Zanzibar.

DSC_1248

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli akiwa amembeba Mtoto Yussuf ambae analelewa katika kituo cha Watoto Mazizini baada ya kuzaliwa na Kutelekezwa na Wazazi wake.katikati ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mama Maudline Cyrus Castico na wa mwisho ni Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mama Shadya  Mohammed Suleiman.

DSC_1277

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli kushoto akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein wapili kulia na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mama Maudline Cyrus Castico katikati wakikabidhi msaada ya Chakula kwa ajili ya Watoto yatima wanolelewa katika Kituo hicho.Wamwisho kulia ni Mkuu wa Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Mjini Unguja.

DSC_1342

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli akipokea Zawadi ya Mkeka kutoka kwa Mlezi wa kijiji cha kulelea Watoto SOS Mombasa Zanzibar,  alipokuwa katika ziara  ya kuwatembelea na kuwafariji Watoto wanaolelewa katika kijiji hicho .

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

About Alex

Check Also

PIX 2

Dkt. Ndungulile : Tujitokeze Kupima Afya Mara kwa Mara.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndungulile …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *