Thursday , March 23 2017

Home / MICHEZO (page 10)

MICHEZO

Habari za Michezo

RONALDO ASHINDA TUZO YA FIFA

buso

Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya FIFA Ronaldo, 31, amewapiku Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid katika sherehe zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi. Ronaldo pia alishinda tuzo ya Ballon d’Or mwezi Disemba mwaka jana, kufuatia mafanikio yake …

Read More »

REKODI YAIBEBA SIMBA DHIDI YA YANGA VISIWANI ZANZIBAR

kotte

  Na.Alex Mathias Timu za Simba na Yanga zote za jijini Dar er salaam, zinatarajiwa kuumana kesho katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Mapinduzi, michezo inayoendelea huko visiwani Zanzibar, hiyo ni kutokana na matokeo ya michezo ya mwisho ya kundi A na kundi B iliyochezwa mwishoni …

Read More »

AZAM FC IMEIPA YANGA KIFURUSHI CHA 4G KOMBE LA MAPINDUZI

bokooo

  Magoli manne ya Azam FC dhidi ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara  yameifanya iongoze kundi B kwa kufikisha pointi saba kombe la Mapinduzi huku ikimaliza mechi yake kwa kishindo cha magoli 4-0 kwenye uwanja wa Amaan visiwani,Zanzibar. Matokeo hayo yanaifanya Azam Fc wafikishe jumla ya pointi …

Read More »

MAN UNITED YAIFUATA MAN CITY HATUA INAYOFUATA YA KOMBE LA FA

reading

Mashetani wekundu Manchester United imesonga mbele katika Michuano ya kombe la Emirates FA baada ya kupata ushindi wa jumla ya magoli 4-0 dhidi ya timu ya Reading inayoshiriki daraja la kwanza mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford mjini Manchester. Nahodha Wayne Rooney alianza kuifungia United dakika ya 7 baada …

Read More »

BONDIA IDDI MKWELA AJIANDAA KUMKABILI MANYI ISSA FEB 5 TAIFA

id

Bondia Iddi Mkwela kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yake wa kujiandaa na kupigana na Manyi Issa Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa ‘Indoor Stadium’ mpambano wa raundi kumi uzito wa KG 61 Picha na SUPER D BOXING NEWS  Bondia Iddi Mkwela akielekezwa …

Read More »

JOHN MIKEL OBI AITEMA CHELSEA NA KUKIMBILIA CHINA

gettyimages-456051316-0

Kiungo wa kati wa Nigeria John Obi Mikel amekuwa mchezaji wa karibuni zaidi kuondoka Chelsea na kuhamia Ligi Kuu ya China. Mikel ametangaza kwenye Twitter kwamba atajiunga na klabu ya Tianjin TEDA. Majuzi, Oscar aliondoka Stamford Bridge na kujiunga na Shanghai SIPG. Mchezaji wa Brazil Ramires alikuwa ameaga klabu hiyo …

Read More »

VISIWANI ZANZIBAR MASHABIKI WAKOSA IMANI NA TIMU ZAO

zeno

Mashabiki mbalimbali wa visiwani Zanzibar kwa upande wao wamesema kwamba hawana matumaini makubwa ya timu moja wapo ya Zanzibar kuweza kufanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ya mapinduzi kwani viwango ambavyo wanavionyesha ni tofauti na timu za Tanzania bara. Mashabiki hao wamesema kwamba timu hizo zinashindwa kufanya vizuri kutokana na …

Read More »

RAIS WA CAF ATUHUMIWA KWA MLUNGULA

fita

Mamlaka zinazosimamia mashindano mbalimbali nchini Misri zimethibitisha kuwa Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF,  Issa Hayatou atafikishwa kwa mkurugenzi  wa mashitaka kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili huku zikiwemo zile za utoaji haki za matangazo ya ligi mbalimbali. Mamlaka hizo zimebainisha kuwa Hayatou alikiuka kipengele namba vifungu (A), (B), (C), (D), (E) za sheria …

Read More »

SIMBA YABANWA MBAVU KOMBE LA MAPINDUZI NA URA YA UGANDA

ura

Na.Alex Mathias. Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba imeshindwa kutamba mbele ya wakusanya mapato toka Uganda timu ya URA baada ya kutoka sare ya 0-0 mchezo wa pili wa Michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar kwenye uwanja wa Amani. Dakika 90 hakuna timu ambayo imeweza …

Read More »

JERRY MURO AIPIGIA MAGOTI TFF

muro

Hatimaye msemaji wa Yanga Jerry Muro ameinua mikono juu na kuiangukia TFF kwa kuandika barua ya kuomba kupunguziwa adhabu ya kufungiwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja. Adhabu ya Muro ilianza Julai 7, 2016 hiyo inamaanisha tayari ameshatumikia adhabu yake kwa kipindi kisichopungua miezi sita. TFF …

Read More »

Diwani Assenga awakumbuka Jellah Mtagwa, Peter Tino

ase2

Diwani Assenga akizungumza na baadhi ya viongozi wa timu shiriki za mashindano ya Diwani Cup Diwani Assenga akikikabidhi jezi kwa  timu shiriki za mashindano ya Diwani Cup ……………………………………………………………………. Na Mwandishi Wetu WACHEZAJI nembo ya Tanzania Kimataifa wanatarajia kuzindua mashindano ya kuwania kombe la Diwani wa Kata ya Tabata, Patrick Assenga …

Read More »

VIJANA ASPIRE KWENDA SENEGAL, VIPAJI VINGINE VYATAFUTWA

jamal-malinzi-1

Vijana watatu wa Tanzania ambao vipaji vyao vilitafutwa katika Mradi wa Aspire, wanatarajiwa kuondoka kesho Januari 5, 2017 kwenda Dakar, Senegal kwa ajili ya kujijunga na Akademi ya Aspire kuendelezwa kwa miaka mitano ijayo. Vijana hao ni Ally Hamis wa Kituo cha Makongo, Dar es Salaam ambaye alizaliwa Septemba 16, …

Read More »

MAANDALIZI YA AIRTEL RISING STARS YAKAMILIKA

airt

Kliniki ya soka ya Airtel Rising Stars iyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa inatarajiwa kuanza Jumatatu, Januari 16 kwenye Uwanja wa Karume huku wavulana 40 na wasichana 25 waliofanya vyema kwenye michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 wakishiriki. Kufanyika kwa kliniki hiyo kutakuwa …

Read More »

MAAMUZI YA GUARDIOLA KUHUSU KUSTAAFU KUFUNDISHA SOKA

pep-guardiola1

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anakaribia kustaafu kufundisha soka na hataitakuwa miaka 65 kama alivyodhani awali. Muispania huyo amewahi kuifundisha klabu ya Barcelona kwa mafanikio makubwa kisha Bayern Munich kabla ya kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini Man city. ”Nitakuwa hapa Manchester kwa misimu ama mitatu labda na zaidi,” Guardiola …

Read More »

LIGI KUU SOKA YA WANAWAKE TANZANIA BARA

karuma

Duru la Pili la Ligi Kuu soka ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajiwa kuanza kesho Jumatano Januari 4, 2017 kwa michezo minne itakayofanyika kwenye viwanja mbalimbali. Kwa mujibu wa ratiba, katika kundi ‘A’ pekee litakuwa na mchezo mmoja wakati kundi ‘B’ litakuwa na michezo mitatu …

Read More »

MWANSASU AANZA KUPATA MATUMAINI YA BEACH SOCER

mwansasu-mbeya

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya mpira wa ufukweni,maarufu kama Beach Socer,John Mwansasu amesema kwamba baada ya wadhamini kuanza kujitokeza kudhamini mchezo huo,anaamini Tanzania itafanya vizuri kwenye michuano mbalimbali. Mwansasu ameyasema hayo baada ya kampuni ya simu ya TTCL kujitokeza kudhamini bonanza la mashindano ya beach soccer kwa vyuo …

Read More »