Thursday , March 23 2017

Home / MICHEZO (page 2)

MICHEZO

Habari za Michezo

MWANJALI NA MNYATE WAZIDI KUITESA SIMBA

Mwajali

Msemaji wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania bara Simba,Haji Manara amesema kuwa beki wao Mzimbabwe Method Mwanjali anaendelea kukosekana kwenye kikosi hicho katika mchezo wa robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Madini FC ya mkoani Arusha utakaochezwa Machi 19 kwenye uwanja wa Sheikh Amani. Mwanjali amekuwa nje …

Read More »

‘YUDA’MOURINHO ‘BADO ANAONGOZA CHELSEA’

DEKO

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amewaambia mashabiki wa Chelsea kwamba yeye bado ni “Number One” (Nambari Moja) baada yake kuzomewa wakati wa mechi ambayo mabingwa hao watetezi wa Kombe la FA walilazwa 1-0 uwanjani wa Stamford Bridge Jumatatu. Mourinho, ambaye alifutwa kazi mara mbili na Chelsea, aliitwa ‘Yuda’ na …

Read More »

MAN UNITED YATEMA KOMBE LA FA CUP DARAJANI

gukp

  Timu ya Manchester United imeshindwa kutetea Kombe lake la FA CUP baada ya kukumbana na kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Chelsea hatua ya Robo Fainali mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge. Hadi Mapumziko hakuna timu iliyokuwa inaongoza kwaani zote zilitoka nguvu sawa kutokana na staili ya mchezo …

Read More »

SERENGETI BOYS WAANZA KAMBI

SERENGETI-BOYS-SA

  Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys imeanza mazoezi rasmi leo Machi 12, 2017 kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Serengeti Boys itakuwa kambini Dar es Salaam hadi Machi 26, mwaka huu ambako …

Read More »

MALINZI AWAPA MAAGIZO MAZITO MAKOCHA WAPYA

Malinzi-TFFvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvv

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amewazawadia makocha wapya 27 waliofuzu kozi ya ukocha kwamba kila mmoja mmoja atampa koni 20 na vizibao 22 kwa ajili ya mazoezi. Rais Malinzi alitoa ahadi hiyo wakati wahafla ya kufunga kozi ya ukocha ngazi ya ‘Intermidiate’ …

Read More »

MALINZI AMLILIA SIR GEORGE KAHAMA

kahama+pic

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, ametuma rambirambi kwa familia ya marehemu Sir George Kahama aliyefariki dunia Jumapili akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. Rais Malinzi amesema taifa limepoteza mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika kupigania maendeleo ya mpira …

Read More »

MAYANGA ATANGAZA KIKOSI CHA TAIFA STARS SURA MPYA ZAINGIA

AMAYA

 Kocha Mkuu wa  timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga ametangaza kikosi chake kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki. Stars inaweza kucheza na kati ya Zambia na Rwanda au timu nyingine kwa kuwa kumekuwa na taarifa tofauti. Lakini kikosi cha Mayanga kiliongozwa na nahodha Mbwana Samatta anayekipiga nchini Ubelgiji …

Read More »

MALINZI KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA KESHO

TOU

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi kesho Jumatatu,Machi 13, 2017 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kufunga kozi ya ukocha ngazi ya ‘Intermidiate’kwa makocha 27 wanaotarajiwa kuhitimu. Kozi hiyo iliyoendeshwa na Wilfred Kidao- Mkufunzi anayetambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), …

Read More »

RATIBA MPYA YA SERENGETI BOYS YATOLEWA

SERENGETI-BOYS-SA

  Wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) likirejesha nyuma kwa wiki moja, timu ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys inatarajiwa kuanza kambi mpya Machi 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Serengeti Boys itakuwa kambini …

Read More »

KAMATI YA NIDHAMU YAIAGIZA TFF

Malinzi-TFF

  Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),imeagiza sekretarieti ya TFF kutoa wito mwingine kwa wanafamilia watatu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) walioshitakiwa mbele ya kamati hiyo. Walioshitakiwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ni Mwenyekiti wa RUREFA, Blassy Kiondo; Mwenyekiti wa …

Read More »

KILA LA KHERI YANGA NA AZAM FC KIMATAIFA

caflogo-Copier

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linazitakia kila la kheri timu za Tanzania, Young Africans na Azam FC ambazo zina mechi za kimataifa zitakazofanyika kesho na keshokutwa. Young Africans ya Tanzania na Zanaco ya Zambia utakaochezwa Jumamosi kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Afrika pia Azam FC ya …

Read More »

MESUT OZIL DONGE NONO-ARSENAL

Mesut-Ozil

Klabu ya Arsenal imepanga kumtengea donge nono la mshahara Mesut Ozil ikiwa ni ofa nono ya mshahara unaofikia paundi 280,000 kwa wiki ili aweze kubakia katika klabu hiyo. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani bado hajaamua kuhusu mustakabali wake huku ikiwa imebaki miezi 15 katika mkataba wake wa sasa, na …

Read More »