Monday , January 21 2019

Home / BURUDANI / WAZIRI NAPE AMKABIDHI TUZO YA HESHIMA DJ BONY LOVE TUZO ZA EATV AWARDS USIKU HUU MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM

WAZIRI NAPE AMKABIDHI TUZO YA HESHIMA DJ BONY LOVE TUZO ZA EATV AWARDS USIKU HUU MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM

1

Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akikabidhi Tuzo ya Heshima kwa DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love baada ya kutangazwa mshindi wa heshima katika tuzo za EATV AWARDS 2016 zilizofanyika  usiku huu  kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.

Tuzo hizo zinaandaliwa na kituo cha Televisheni cha EATV cha jijini Dar es salaam kinachorusha matangazo yake katika nchi za Afrika Mashariki.

2

DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love akipongezwa na DJ John Dilinga mara baada ya kupokea tuzo yake ya Heshima katika tuzo zilizoandaliwa na Kituo cha Televisheni cha EATV.

3

DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love akizungumza machache huku rafiki yake John Dilinga akiwa ameshika tuzo hiyo.

4

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akimsikiliza DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love alipokuwa akitoa shukurani zake mara baada ya kupokea tuzo yake ya heshima iliyotolewa na EATV.

5

Mwanamuziki Lady Jay Dee akipongezwa na mumewe. mara baada ya kupokea tuzo yake  katika hafla ya utoaji wa tuzo za  EATV AWARDS zilizofanyika kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.

1

Mwanamuziki Ali Kiba akipokea tuzo yake ya ushindiwa Wimbo Bora wa Mwaka kutoka kwa Nandi Mwiyombela Mkuu Masoko na Mawasiliano  kampuni ya Vodacom Tanzania katika Tuzo za Muziki za EATV AWARDS zinazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

2

Mwanamuziki Ali Kiba akizungumza mara baada ya kupokea tuzo yake.

3

Mwanamuziki Vanessa Mdee akifanya vitu vya ke jukwaani wakati wa utoaji wa tuzo hizo.

4 5

Mshindi wa filamu bora ya mwaka anayejulikana kwa jina la Gabo akizungumza mara baada ya kupokea tuzo yake usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

6

Mwanamuziki Lady Jay Dee akitumbuiza katika tuzo hizo.

1

Mwanamuziki Vanessa Mdee pamoja na mpenzi wake Jux wakipiga picha kwenye Red Carpet wakati walipowasili kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam kushuhudia tuzo za EATV AWARDS 2016 zinazofanyika usiku huu.

3 4

Mwanamuziki  Dully Sykes na mtangazaji wa Clouds Babu wa Kitaa wakihojiwa na mwandishi wa habari wakati walipowasili kwenye ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya Tuzo za EATV AWARDS 2017.

5

Wageni waalikwa mbalimbali wakiwasili katika ukumbi huo.

6

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa na Mkurugenzi wa EATV Regina Mengi na Katibu Mtendaji wa BASATA John Mngereza kulia.

7

Red Carpet likipitiwa

8

Picha pia zikapigwa kama unavyoona katika picha.

10

Pozi zikaongezaka ilimradi raha tu.

11

Nandi Mwiyombela Mkuu wa Masoko na Mawasiliano kutoka kampuni ya simu ya Vodacom akiwa pamoja na waalikwa wengine katika tuzo hizo.

12

Waziri wa Habari , Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Nnauye  akizungumza na Regina Mengi Mkurugenzi Mtendaji wa EATV inayoandaa tuzo hizo.

13

Baadhi ya waalikwa wakiwa katika tuzo hizo.

14

Mamia ya waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.

15

About bukuku

Check Also

image

NGOMA AFRICA BAND NA CD YAO MPYA AWAMU YA TANO HAPA KAZI

Si wengine ni hile bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × 1 =