Wednesday , January 17 2018

Home / MICHEZO / DOMAYO AIPELEKA AZAM FC FAINALI MAPINDUZI CUP,YAISUBIRI SIMBA AU YANGA

DOMAYO AIPELEKA AZAM FC FAINALI MAPINDUZI CUP,YAISUBIRI SIMBA AU YANGA

clement-bedo-r-of-malakia-fc-challenges-frank-domayo-of-azam-fc_1nc8a1dh974xx17m871v55k1bm

Na.Alex Mathias.

Bao la kiungo mkabaji wa zamani wa Yanga,Frank Domayo dakika ya 33 limeipeleka Azam FC Fainali ya Michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar kwenye uwanja wa Amaan.

Frank Domayo aliachia shuti la mita 18 na kumuacha mlinda mlango wa Taifa Jang’ombe akiwa hana la kufanya na kupelekea timu hizo kwenda mapumziko Azam Fc wakiwa wanaongoza kwa bao hilo.

Kipindi cha pili kilianza kwa Taifa Jang’ombe kulishambulia lango la Azam kama nyuki huku wakikosa nafasi nyingi wakati Matajiri wa jiji la Dar es salam wakicheza kwa mashambulizi ya kushtukiza huku wakilinda bao lao.

Baada ya kuona kosakosa nyingi timu zote zilifanya mabadiliko mbalimbali hata hivyo mabadiliko hayo hayakuwasaidia Jang’ombe na kukubali kipigo toka kwa Azam ambao wametinga Fainali itakayochezwa siku ya Ijumaa ya Januari 13,2017.

Kwa Matokeo hayo Azam wanasubiri mshindi kati ya mahasimu wa kariakoo Simba na Yanga ambao wanatarajia kumenyana majira ya saa 2:15 kwenye uwanja huo huo wa Amaan.

Ngoja tusubiri ni Simba au Yanga atakwenda kucheza na Azam FC Fainali ya 11 ya Kombe la Mapinduzi ya mwaka 2017 ambapo tayari bingwa mtetezi alishavuliwa ubingwa na timu ya Taifa ya Jang’ombe.

About Alex

Check Also

IMG_0024-750x350

SEKRETARIETI YA TFF YAWASHTAKI WANNE KWENYE KAMATI YA MAADILI

  Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fifteen − 14 =