Wednesday , January 17 2018

Home / MICHEZO / KOMBE LA DUNIA KUWA NA TIMU 48

KOMBE LA DUNIA KUWA NA TIMU 48

ukf

Shirikisho la Soka Duniani Fifa limeidhinishwa mpango wa kupanua Kombe la Dunia liwe linashirikisha mataifa 48.

Mpango huo utaanza kutekelezwa Kombe la Dunia la 2026, na unatarajiwa kufaidi Afrika na Asia.

Chini ya mpango ulioidhinishwa, kutakuwa na makundi 16 ya mataifa matatu kila kundi, ambapo mataifa mawili bora yataingia hatua ya muondoano ya timu.

Mpango huo ambao umekuwa ukipigiwa debe na rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino uliidhinishwa kwa kauli moja na wanachama wa Fifa mjini Zurich Jumanne.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kupanuliwa tangu mwaka 1998.

Kulikuwa na mapendekezo matano ambayo baraza kuu la Fifa lenye wanachama 37 lilikuwa linaangazia.

  • Kombe la Dunia lenye timu 48 na makundi 16 ya timu tatu kila kundi ambapo timu mbili bora zitasonga kwa hatua ya muondoano ya timu 32 (mechi 80 kwa jumla).
  • Kombe la Dunia la timu 48, mechi moja ya muondoano wa kufuzu ambapo mshindi atajiunga na timu 16 nyingine (mechi 80 kwa jumla – 16 za muondoano wa kufuzu na 64 za michuano kamili).
  • Kuwa na timu 40 na makundi 10 ya timu nne kila kundi ambapo mshindi, na timu sita pekee zinazomaliza nambari mbili kundi ndizo zinafuzu (makundi 76).
  • Kuwa na timu 40 na makundi manane ya timu tano kila kundi (mechi 88).
  • Kusalia na Kombe la Dunia lilivyo sasa ambapo kuwa timu 32 (mechi 64).

Infantino, 46, ambaye alimrithi raia mwenzake Sepp Blatter kama rais wa Fifa mwezi Februari 2016 alifanya kampeni akiahidi kupanua michuano hiyo.

Awali alipendekeza michuano ya timu 40, wazo lililowasilishwa na rais wa wakati huo wa Uefa Michel Platini 2013, kabla ya kubadilisha msimamo na kuunga mkono michuano ya timu 48.

ifo

Chini ya mpango wa Infantino alioupendekeza kwa sasa, mechi zinaongezeka kutoka 64 hadi 80, lakini fainali bado zinaweza kuchezwa kwa kipindi sawa na cha sasa cha siku 32.

Taifa halitatakiwa kucheza zaidi ya mechi saba, sawa na ilivyo chini ya mpango wa sasa.

Udhaifu pekee ni kwamba huenda mikwaju ya penalti ikatakiwa kutenganisha klabu zinazotoka sare kwenye makundi.

About Alex

Check Also

IMG_0024-750x350

SEKRETARIETI YA TFF YAWASHTAKI WANNE KWENYE KAMATI YA MAADILI

  Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × three =