Wednesday , January 17 2018

Home / MICHEZO / TUJIFUNZE KUUHESHIMU MPIRA

TUJIFUNZE KUUHESHIMU MPIRA

 

ctqpziwweaahr7b

Imani Kelvin Mbaga

Ni asubuhi ya tarehe 10 mwezi January ambapo kurasa za michezo kwenye magazeti, vipindi mbalimbali vya michezo kwenye vyombo vya habari vya ki electoniki, mazungumzo ya wapenda soka katika vijiwe mbali mbali, bila kusahau mitandao ya kijamii, mada kubwa ya leo ni mpambano wa watani wa jadi, Simba na Yanga katika kombe la mapinduzi, mchezo wa nusu fainali utakaochezwa leo usiku.

Kila shabiki anauzungumzia kwa namna yake, kwa matumaini makubwa, hamasa na bashasha nyingi jambo ambalo halikatazwi na ni sehemu ya starehe ya mpira wa miguu.

Napenda kukukumbusha mambo machache shabiki mwenzangu ili yawe silaha yako kabla na baada ya dakika 90.

Kwanza mpira ni mchezo usio tabirika, ni ngumu sana kujua kwa uhakika matokeo ya mwisho ya mchezo, waulize watu wanao beti watakuambia.

Pili mpira ni mchezo wenye matokeo ya kikatili, kwani kuna wakati haukupi matokeo halisi ya unachokiona, anaemiliki mpira kwa kila eneo mwisho wa siku unaweza ukakuta anapoteza

Kubwa zaidi matokeo ya mpira yanategemea mambo mengi zaidi ya mchezo wenyewe na baadhi ya vitu vinavyochangia matokeo ni kama, bahati, maamuzi, maandalizi (hapa ni pamoja na ufundi), mood ya wachezaji, makosa ya kiufundi, hali ya hewa na juhudi binafsi.

Ukisoma, kusikiliza watu wanasemaje utagundua wote wanaingia uwanjani leo na asilimia mia ya uhakika wa ushindi mwisho wa siku atakaepoteza akubali tu msianze kutafuta mchawi kama utamaduni wenu ulivyo

Niwatakie mchezo mwema utabiri wangu nitautoa kesho kutwa post zenu nimezihifadhi mjue

About Alex

Check Also

IMG_0024-750x350

SEKRETARIETI YA TFF YAWASHTAKI WANNE KWENYE KAMATI YA MAADILI

  Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eleven − seven =