Wednesday , January 17 2018

Home / BURUDANI / WAZIRI NAPE NA DStv WAONGEZA NGUVU SHOO YA DIAMOND PLATINUM UFUNGUZI WA AFCON NCHINI GABON

WAZIRI NAPE NA DStv WAONGEZA NGUVU SHOO YA DIAMOND PLATINUM UFUNGUZI WA AFCON NCHINI GABON

dstv-nape

Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na sanaa Kushoto,Diamond Platnumz katika pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania bw.Salum Salum.

dstv-nape-6

Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania Shumbana Walwa akiwa anaongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kumkabidhi Diamond Platnumz bendera ya Tanzania kuelekea katika ufunguzi wa Afcon nchini Gabon.

dstv-nape-3

Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Bw.Alpha Joseph akimkalibisha Kaimu Mkurugenzi Salum Salum katika hafla ya utoaji wa Bendera kwa msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz.

salum

Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Bw.Salum Salum akimkaribisha mgeni wa tukio ambaye ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Michezo na Sanaa Mh.Nape Nnauye hayupo pichani.

dstv-nape-1

Waziri wa Habri,Michezo,Utamaduni na Sanaa Mh.Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari wakati wa kumkabidhi Bendera Diamond Platnumz anayekwenda kwenye shoo ya Ufunguzi wa Afcon nchini Gabon.

dstv-nape-8

Msanii Diamond Platnumz akitoa shukruni kwa Serikali na DStv pamoja na waandishi wa habari kwa mchango wao pamoja na kuendelea kumsapoti kupitia kazi zake.

dstv-nape-5

Mh.Nape Nnauye akisalimiana na Msanii Diamond Platinum.

dstv-nape-7

Msanii wa vichekesho nchini Tanzania JOTI ambaye pia ni balozi wa Kifurushi cha DStv Bomba ambacho kitarusha moja kwa moja Michuano ya Afcon akitoa pongezi kwa Kampuni ya Multichoice Tanzania.

dstv-nape-4

Waziri wa Habari,Utamaduni,Michezo na Sanaa Mh.Nape Nnauye katika akiwa na balozi wa kifurushi cha Bomba Joti kulia pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Bw.Salum Salum kushoto wakiteta jambo.

dstv-nape-11

Baadhi ya Waandishi waliohudhuria tukio hilo wakiwa katika majukumu yao ya kuchukua picha.

dstv-nape-13

Msanii Diamond Platinum akiwa na bendera baada ya kukabidhiwa na Serikali tayari kuelekea kwenye ufunguzi wa Michuano ya Afcon inayoanza Jumamosi ya Januari 14.

dstv-nape-12

Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Nape Nnauye pamoja na Msanii Diamond Platinum.

PICHA NA MO DEWJIBLOG.

………

Kuelekea katika Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika ‘AFCON’ Kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia Kifurushi cha DStv Bomba imetoa tiketi sita kwa vijana wa Msanii wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum kwenda kushuhudia ufunguzi huo.

Ufunguzi huo wa michuano hiyo mikubwa Afrika, inatarajiwa kufanyika Januari 14, mwaka nchini huko ambako Dimaond amealikwa kwenda kutuimbuza.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alimkabidhi bendera ya taifa, Diamond kwa ajili ya kwenda kuipeperusha vyema Tanzania katika ufunguzi huo.
“Kikuweli nimpongeze Diamond kwa mwaliko alioupata wa kwenda kutumbuiza kwenye michuano mikubwa Afrika ya Afcon, siyo kitu kidogo kwake, ni nafasi ya yeye kujitangaza zaidi kimataifa, ninaamini wapo wasanii wengi wazuri Afrika, lakini kachaguliwa yeye hivyo anastaili pongezi,” alisema Nape.
Nape ndiye aliwaomba DStv kujitokeza na kudhamini safari ya wachezaji shoo wa Diamond na baadhi ya watu wa timu yake kwenda Afcon ili kuhakikisha anafanya shoo ya uhakika zaidi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DStv, Salum Salum alisema wametoa tiketi hizo kwa Diamond kwa lengo kukuza na kuendeleza vema tasnia ya filamu.
“Tunathamini tasnia ya sanaa nchini kwa kupitia muziki na filamu, hivyo basi katika kutambua hilo tumetoa tiketi sita kwa kundi la WCB chini ya msanii Dimaond kwa ajili ya kwenda kwenye uzunduzi wa Afcon huko Gabon.
“Tumempatia tiketi hizo, baada ya kuomba udhamini wa tiketi hizo kwa ajili ya vijana wake sita atakaombatana nao kwenye shoo hiyo na kikubwa tunataka kuona Diamond anafunika ili atauwakirishe vema,” alisema Salum.
DStv, ndiyo itaonyesha michuano hiyo mikubwa ya kimataifa kwa kifurushi chake cha bei cha chini kabisa kitakachopatikana kwa Shilingi 19, 975 tu.

About Alex

Check Also

2

DStv YAONGEZA TAMTHILIA ZA KITANZANIA!

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harishon Mwakyembe(katikati) na Katibu Mtendaji wa Bodi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 + 2 =