Thursday , March 21 2019

Home / BIASHARA / PSPTB YAENDESHA MAFUNZO YA SIKU 5 YA UTAFITI KWA WANAFUNZI WANAOTARAJIWA KUFANYA MITIHANI YA BODI HIYO

PSPTB YAENDESHA MAFUNZO YA SIKU 5 YA UTAFITI KWA WANAFUNZI WANAOTARAJIWA KUFANYA MITIHANI YA BODI HIYO

1

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akizungumza na wanafunzi waliofikia  Level 5 wanaotarajiwa kufanya mitihani ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi Ugavi  katika Warsha ya Mafunzo ya siku ya  Utafiti iliyondaliwa na Bodi hiyo ambapo kila mwanafunzi atapangiwa msimamizi wa utafiti wake na baadaye utafiti wao utapimwa kitaalamu  ambapo  utawawezesha kuwa wataalamu wa masuala ya Ununuzi wa Umma baada ya Kupata cheti cha kitaaluma cha (CPSP)

Bw. Godfred Mbanyi amewataka  wanafunzi hao kuwa wasikivu wakati wa mafunzo  hayo, lakini pia amewaasa kuwa na maadili ya kazi zao,  Amesema pamoja na kusoma na  kuwa na vyeti lakini kama hawatakuwa na maadili hawatakuwa na umuhimu wowote kwa bodi na kwa nchi kwa ujumla.

Mbanyi ameongeza kwamba “Wakimalizia mitihani yao na kufaulu tutawaapisha kiapo cha maadili na Utii na kiapo hicho tutakitumia mahakamani kama ushahidi endapo hawatafuata maadili katika kazi zao na kuifedhehesha Bodi ya (PSPTB) kwa kufanya mambo bila kufuata utaratibu wa sheria zinazozimamia Ununuzi wa Umma”.

Amemaliza  na kusema kwamba Wataalamu wa masuala ya Ununuzi wa Umma wanashikilia fedha nyingi za serikali lakini watambue kwamba fedha hizo ni za watanzania na wanatakiwa kuzitumia vizuri kwa kufuata utaratibu uliowekwa ili ziwe na  manufaa kwa watanzania wote katika kuondokana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo ya nchi na watanzania kwa ujumla, warsha hiyo inafanyika kwenye ukumbi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es salaam

  3

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani ya Ununuzi wa Umma iliyofanyika kwenye ukumbi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es salaam, Kulia ni Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB) na kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk Ikandilo Kushoka.

4

Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB) akizungumza katika warsha hiyo katikati ni Bw. Godfred Mbanyi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (PSPTB)  na kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk Ikandilo Kushoka.

5

Bw. Godfred Mbanyi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (PSPTB)  akifafanua jambo katika warsha hiyo  kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk Ikandilo Kushoka na kulia ni Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB).

6

Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa PSPTB Bw. Godferd Mbanyi hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza nao.

7 9 8

Wanafunzi hao wakisikiliza kwa makini

10

Wakifuatilia warsha hiyo kwa umakini mkubwa.

About bukuku

Check Also

maxresdefault

HOTELI YA KWANZA ARUSHA YATENGA MILIONI KUMI KWA AJILI YA YATIMA

UONGOZI wa hoteli ya kitalii ya New Safari Hoteli ya jijini Arusha umefanikiwa kujiwekea utaratibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

one × four =