Saturday , March 23 2019

Home / MICHEZO / STAR MEDIA TANZANIA YACHANGIA SERENGETI BOYS

STAR MEDIA TANZANIA YACHANGIA SERENGETI BOYS

1 2

Kampuni ya Star Media Tanzania imekabidi hundi ya shilingi milioni ishirini (20) kwa Waziri Wa Habari Utamaduni Na Michezo Dk.Harisson Mwakyembe katika harambee ya kuchangia timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka kumi na saba Serengeti Boys iliyofanyika April 30, 2017 katika ukumbi wa JK Nyerere Convetion Center.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa StarTimes Tanzania  Mr.Wang Xiaobo amesema kuwa “Tunafuraha kubwa sana kuichangia Serengeti boys  pamoja na serikali katika jitihada za kukuza michezo nchini,Tunaitakia timu kila la kheri iweze kuwakilisha vema nchi katika medani za kimichezo”

Ameongeza kuwa mafanikio ya baadae yanategemea msingi mzuri na uwekezaji mzuri  kwa vijana kwani ni hazina nzuri na tegemeo la kesho kwa kuliletea mafanikio taifa.Mbali na uchangiaji huu tutaendelea kuchangia michezo mingine pamoja na shughuli za kiuchumi na kijamii ili kuisaidia nchi katika jitihada zake za kuleta maendeleo kwa wananchi.

Akiongea Waziri wa Habari,Utamaduni ,michezo na Sanaa Dk.Harrison Mwakyembe amewashukuru  Star Media Tanzania na ameahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau kaika kufanikisha malengo yao na pia michezo kwa ujumla .

Pia,Ameongeza kuwa bado sekta ya michezo inakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini wizara yake itaendelea kurekebisha ikishirikiana na wadau wengine ili kuleta mabadiliko katika sekta hii.

About Alex

Check Also

NGEREJA 4D

MATUKIO KATIKA PICHA :UONGOZI WA BUNGE SPORTS CLUB WAITAKIA HERI TIMU YA TAIFA STARS

Mwenyekiti wa Timu ya Michezo ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngereja akizungumza na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

8 + fifteen =