Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

RPC MWANZA

  • WATU WAWILI WAMEUAWA NA FISI NA WENGINE WATANO KUJERUHIWA WILAYANI SENGEREMA.
  • MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATINA AKIWA NA NOTI BANDIA WILAYANI NYAMAGANA.

KWAMBA TAREHE 01.05.2017 MAJIRA YA SAA 9:00HRS KATIKA KIJIJI CHA NYASHANA KATA YA KALEBEZO WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LUCIA SINZA, MIAKA 65, MKULIMA WA KALEBEZO NA 2. MTOTO MDOGO AITWAYE JUMA AMOS MIAKA 3 ,  WAKIWA SHAMBANI WALIVAMIWA NA KUSHAMBULIWA NA FISI NA KUPELEKA  KUPOTEZA MAISHA  PAPO HAPO HUKU WATU WENGINE WATANO WAKIJERUHIWA WAKATI WALIPOFIKA KUWAOKOA.

INADAIWA KUWA WAKATI WAKIWA SHAMBANI ALITOKEA FISI ALIYEMVAMIA MAREHEMU BI LUCIA SINZA NA KUMWANGUSHA CHINI KISHA KUANZA KUMNG’ATA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE, INADAIWA WAKATI FISI AKIENDELEA KUMSHAMBULIA BIBI LUCIA  MTOTO  WAKE ALIYEKUWA NAYE SHAMBANI HAPO AITWAYE KEFRENI FAIDA ALIKWENDA KUMSAIDIA MAMA YAKE, NDIPO FISI ALIMUACHA BI LUCIA KISHA ALIMRUKIA KEFRIDA SAIDA LAKINI KWA BAHATI MBAYA ALIMNG’ATA KICHWANI MTOTO ALIYEKUWA AMEMBEBA MGONGONI AITWAYE JUMA AMOS NA KUPELEKEA JERAHA KUBWA  LILILOSABABI KUPOTEZA MAISHA HUKU MAMA WA MTOTO KEFRENI FAIDA AKIJERUHIWA MKONO NA SEHEMU YA JUU YA PAJA LA MGUU WA KUSHOTO.

KUTOKANA NA KUSIKIKA MAYOE/KELELE KUTOKA SEHEMU HIYO WATU/ MAJIRANI WALIFIKA ENEO LA TUKIO KUTOA MASAADA LAKINI BAADHI YAO PIA WALIJERUHIWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO AMBAO NI 1.SOSTENES KISUMU MIAKA 25, ALIJERUHIWA MKONO WA KULIA NA PAJI LA USO, 2.TEKLA LUNILIJA MIAKA 60, ALIJERUHIWA MKONO WA KULIA, 3.ABELI WILIAM MIAKA 35, ALIJERUHIWA MGUU WA KUSHOTO NA 4.MUSA NYUMA MIAKA 40, ALIYEJERUHIWA KISHA KUTOLEWA KIGANJA CHOTE CHA MKONO WA KULIA.

ASKARI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA KUFANYA MSAKO MKALI WA KUMTAFUTA FISI HUYO NA KUFANIKIWA KUMUUA, AIDHA MAJERUHI WANAENDELEA NA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA SENGEREMA NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI, MIILI YA MAREHEMU TAYARI IMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA POLE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIOPATWA NA MSIBA HUO, LAKINI PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUWA WAVUMILIVU KATIKA KIPINDI HIKI KUGUMU, AIDHA ANAWAOMBA WANANCHI KUWA MAKINI PINDI WANAPOKUWA KATIKA MAENEO YA MASHAMBANI DHIDI YA WANYAMA WAKALI WANAOWEZA HATARISHA MAISHA YAO, NA PALE WANAPOONA WANYAMA WAKALI KATIKA MAENEO YAO WATOE TAARIFA HARAKA KWA VIONGOZI WA VIJIJI/KATA NA VYOMBO VYA DOLA.

KATIKA TUKIO LA PILI,

MNAMO TAREHE 29.04.2017 MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONI KATIKA MAENEO YA KITUO CHA MABASI YA NYEGEZI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA TUMAINI FRANK MIAKA 27, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MAJENGO MAPYA NYEGEZI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA TISA ZA SHILINGI ELFU KUMI ZENYE JUMLA YA TSH 90,000/=, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.

AWALI INADAIWA KUWA WANANCHI WALIMTILIA MASHAKA MTUHUMIWA KUWA ANAMILIKI NOTI BANDIA, NDIPO BAADHI YA WATU WALIKWENDA KUMKAMATA MTUHUMIWA KISHA WAKAMPELEKA KWENYE KITUO CHA POLISI.  AIDHA BAADA YA KUFIKISHWA KITUONI  HAPO ASKARI WALIMFANYIA UPEKUZI MTUHUMIWA NA KUFANIKIWA KUMKAMATA AKIWA NA NOTI BANDIA TISA ZA SHILINGI ELFU KUMI.

MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, UPELELEZI NA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOSHIRIKINA NA MTUHUMIWA KATIKA KUTENDA UHALIFU HUO BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWAOMBA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA DHIDI YA WAHALIFU KATIKA MAENEO YAO, LAKINI PIA ANAWAPONGEZA BAADHI YA WANANCHI WALIOMKAMATA MTUHIMIWA NA KUMFIKISHA KITUO CHA POLISI BILA KUJICHULIA SHERIA MKONONI, HIVYO ANAOMBA SUALA HILO LIWE SOMO KWA WATU WENGINE KWAMBA PINDI WANAPOMKAMATA MHALIFU WAMFIKISHE POLISI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHULKULIWA DHIDI YAKE NA SIO KUJICHULIA SHERIA MKONONI.

IMETOLEWA NA:

DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 × 1 =