Tuesday , January 22 2019

Home / SIASA / WAZEE WA CCM Z’BAR WATOA WAMPONGEZA DR.SHEIN NA KUTOA MAPENDEKEZO MAZITO.

WAZEE WA CCM Z’BAR WATOA WAMPONGEZA DR.SHEIN NA KUTOA MAPENDEKEZO MAZITO.

Q
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CCM Zanzibar, Bi.Khadija Jabir akizungumza na waandishi wa Habari juu ya kumpongeza Dkt.Shein huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui .
Q 1
Mmoja wa Wazee wa Chama hicho, Bw. Haji Machano akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya kikao hicho.
Q 2
Baadhi ya waandishi wa habari na Wazee mbali mbali walioudhuria mkutano huo.
……………..
Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kwa niaba ya wazee wote wa Chama hicho linampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein kwa kutimiza ahadi yake ya kuinua kiwango cha chini cha Mishahara 100% kwa watumishi wa Umma, hatua iliyoanzia mwezi wa April, 2017.

Pia wamemuomba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuendelea kusimamia kwa umakini mambo yafuatayo:-

1.Kuwabana wasiolipakodi hasa baadhi ya wafanyabiashara wenye tabia za ukwepaji wa kodi hizo.

2. Kusimamia Bodi zinazoshughulikia masuala ya upandaji wa bei za bidhaa ili kuzuwia mfumko wa bei hizo zinazopanda bila ya kuzingatia kipato cha wananchi.

3. Pia, Afanye tathmini zitakazosaidia kusimamia rasli mali za Zanzibar ili zitumike kwa uangalifu zaidi kwa kuwanufaisha wananchi wote.

Aidha, tumefurahishwa na tukio la kupunguza kodi ya mapato kutoka kiwango cha asilimia 13% hadi asilimia 9% Lakini pia kusimamia na kuwajibisha watendaji wasio waaminifu kwa Serikali.

Pamoja na pongezi zetu wazee tunatoa nasaha kwa watumishi wa Umma kwa kuwaomba wafanye kazi kwa bidii na uadilifu. Mwisho sisi wazee tunawatakia mema wafanyakazi wa SMZ katika maisha yao na tunamuombea Mhe. Rais Dk. Ali Mohamed Shein na familia yake maisha mema, afya bora na mafanikio makubwa.

                                                                                                     AHSANTENI SANA
                                                                                          KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
                                                                                                    MAPINDUZI DAIMA
                                                                                                         CCM OYEE!
                                      

                                                                                                    (KHADIJA JABIR)
                                                                          MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE WA CCM
                                                                                                    ZANZIBAR
                                                   
                                                                                                       02/05/2017

About Alex

Check Also

IMG_1892

UVCCM WAJENGA TAWI LA CCM KANGANI

NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar ndugu Mussa Haji Mussa(kushoto), Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 + twenty =