Tuesday , November 21 2017

Home / MCHANGANYIKO / Wakuu Wa Nchi Za Afrika Mashariki Kukutana kesho Dar

Wakuu Wa Nchi Za Afrika Mashariki Kukutana kesho Dar

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

WAKUU wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajia kufanya mazungumzo ya pamoja baina yao katika  Mkutano wa kawaida wa  18 utakaofanyika kesho Mei 20 Ikulu jijini Dar es salaam.

 

Mkutano huo unatarajiwa kupokea  ripoti ya usuluhishi ya kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamini William Mkapa kuhusu mgogoro wa nchini Burundi.

 

Mambo mengine yatakayozungumzwa katika mkutano huo ni pamoja na taarifa na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa katika mkutano wa 17 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo.

 

Masuala hayo ni pamoja na namna ya kuwezesha uundaji wa magari katika   Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupunguza uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka nje ya Jumuiya, mapitio kuhusu sekta ya nguo na ngozi.

Aidha masuala mengine ni pamoja na  kuzuia ama kuondoa uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika   kutoka nje.

Wakuu hao wa Nchi pia wanatarajia kujadili namna endelevu ya uchangiaji wa bajeti ya Jumuiya hiyo kwa nchi wananchama.

Aidha, katika Mkutano huo wa 18 Tanzania itakabidhi  nafasi ya mwenyekiti wa Jumuiya hiyo iliyoishika kwa muda wa miaka miwili kwa nchi ya Jamhuri ya Uganda.

 

About Alex

Check Also

1

TANZANIA YAPIGWA MSASA NA ISRAEL WA KUTANGAZA UTALII KIDIGITALI

Dr. Noam Koriat akitoa mafunzo kwa watumishi wa Wizara ya Utalii na Taasisi zake katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × 3 =