Tuesday , January 22 2019

Home / BURUDANI / CHIN BEES AACHIA WIMBO NA VIDEO MPYA ‘NYONGA NYONGA’

CHIN BEES AACHIA WIMBO NA VIDEO MPYA ‘NYONGA NYONGA’

JAM

Baada ya kujitengenezea heshima adimu kama ‘Prince wa Trap’ Tanzania kupitia ngoma yake, Pepeta, Chin Bees ameachia wimbo mpya ‘Nyonga Nyonga’ pamoja na video yake.

Wimbo huo wenye mahadhi ya dancehall iliyochanganyikana na ladha za aina yake za Kibongo, unadhihirisha uwezo wa Chin katika kubadilika kwenye mahadhi mbalimbali kama atakavyo. Nyonga Nyonga ambao ni wimbo wa pili wa rapper huyo akiwa chini ya usimamizi wa label ya Wanene Entertainment.

 “Ni dancehall lakini za watu fulani ambao wamezimiss. Ni muziki fulani tofauti ambao hata mtu akisikiliza lazima atabounce,” anasema. Ameongeza, “It’s a typical African hit na ikishakuwa hivyo inaweza kusikilizwa kokote Afrika kwasababu nilichokifanya ni vitu ambavyo viko musical, kote duniani wanaweza wakafeel. It’s a new tone,” anasema.

“Nimewaletea watu kitu ambacho ni tofauti ambacho kitawafanya wacheze na mind zao ziwe fresh kwa kusikiliza.”

Wimbo huo umetayarishwa na Dr.Reggy, mpishi ambaye amewahi kufanya miradi mingi na Chin Bees siku za nyuma. “Dr.Reggy ni producer wangu wa kwanza kabisa, nimeanza kufanya naye kazi kitambo kabla hata sijawa na jina kubwa,” anafafanua.

Video ya wimbo huo imefanyika katika mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam huku rangi za nguo walizovaa wote wanaoonekana, zikitengeneza picha ya kuvutia machoni na yenye Uafrika mwingi.

Kuhusiana na video hiyo Chin amesema, “Imefanyika hapa hapa Wanene na tuliamua kuifanyia nje zaidi tofauti na video yangu iliyopita ya Pepeta ambayo yote ilifanyika ndani. Tumefanya kwenye yale mazingira ya mtaani kabisa.”

“Theme ya video ilikuwa ni kuonesha rangi za mtaani na mavazi pamoja na mazingira halisi ya Kitanzania na yenye muonekano wa kizamani,” anasema Director H aliyeiongoza video hiyo.

Nguo hizo zimebuniwa na mbunifu wa mavazi, Samuel Sebedayo (SAMZ) huku Rehema Samo akihusika kwenye styling.

Nyonga Nyonga ni wimbo unaotarajiwa kuwa katika albamu ya kwanza ya Chin Bees iliyopangwa kuachiwa baadaye mwaka huu.

Kuangalia video ya Nyonga Nyonga, bofya hapa: https://www.youtube.com/watch?v=-z0HGHpMEwo&feature=youtu.be

Kupakua wimbo bofya hapa: http://bit.ly/NyongaNyonga

About bukuku

Check Also

image2

TAMTHILIA YA ”WILDFLOWER” INAREJEA KWA MSIMU WA PILI KWENYE ST NOVELA E PLUS

Tamthilia kali ya Wildflower inarudi tena kwenye king’amuzi cha StarTimes. Msimu wa pili wa tamthilia …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

12 − 9 =