Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo azindua Mradi wa maji Ngorongoro

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo azindua Mradi wa maji Ngorongoro

Mkuu wa mkoa Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amezindua mradi mkubwa wa maji wa maji kwaajili ya kunyweshea mifugo(cattle trough) na matumizi ya binadamu katika kata ya Ndepes wilayani Ngorongoro.
Mradi huo mkubwa wa maji umetumia takribani milioni 200 ikiwa ni gharama nzima za mradi huo, utekelezaji wa mradi huo umesimamiwa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni utekelezaji wa agizo la waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa mapema mwezi wa Desemba 2016, moja ya maagizo yake ilikua ni wananchi kujengewa mfumo wa maji kwa matumizi yao na mifugo yao ili kuzuia  uingizwaji wa mifugo katika crater ya Ngorongoro.
Aidha Mhe. Gambo ameipongeza mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kuutekeleza mradi huo kwa wakati na kuendelea kutoa msisitizo kwa wananchi kuwa agizo la kutoingiza mifugo ndani ya crater linaendelea na amezitaka mamlaka kuanza mchakato wa kuligeuza agizo hilo kuwa sheria ili liweze kutekelezeka kwa vitendo zaidi.
Wananchi wa eneo la Ndepes wameishukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ahadi yake ya kuhakikisha wananchi hawafuati maji umbali zaidi ya mita mia nne kama ilivyo ahidiwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

About bukuku

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

18 − 6 =