Monday , January 21 2019

Home / BIASHARA / NEEC, UN, HDIF Wazindua Mafunzo Kwa Wajasiriamali

NEEC, UN, HDIF Wazindua Mafunzo Kwa Wajasiriamali

 


Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji,Bengi Issa, akizungumza na waandishi wa habarai Dar es Salaam jana wakati wa semina kwa vijana kuhusu namna ya kutumia Fursa kujikwamua kiuchumi. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez,Mkurugenzi wa Fursa, Ruge Mutahaba na Kiongozi wa Shirika la Maendeleo ya Jamii na Ubunifu Endelevu (HDIF),David McGinty.


,Mkurugenzi wa Fursa, Ruge Mutahaba akifafanua jambo mbele ya Waandishi
wa habarai jijini pichani kati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji,Bengi Issa

Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Umoja wa Mataifa (UN) na shirika la Human Development Innovation Fund (HDIF) leo wameungana na kuzindua mafunzo ya aina tano za ujuzi kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata mbinu bora za ujasiriamali mdogo na wa kati hapa nchini Tanzania.

Misingi ya ujuzi na mbinu hizi inalenga kukuza na kuboresha uzoefu wa vijana katika ujasiriamali. Ujuzi huu utawasaidia kuwa imara na kuweza kuhimili ushindani wa kiuchumi.

Mafunzo haya yenye mbinu tano yatalenga ukuzaji wa bidhaa, mauzo, kumbu kumbu za mauzo, ujuzi wa kawaida pamoja na taratibu na sheria za kufanya kazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Bw. Beng’i Issa alisema anaamini ya kwamba uzinduzi wa mafunzo haya yatasaidia Taifa kufanikisha malengo ya kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2015.

Kuendeleza wajasiriamali ni muhimu sana kama kweli Tanzania ina lengo la kuwa nchi ya viwanda. Wajasiriamali watajenga fursa nyingi ambazo zitatoa ajira kwa watanzania na kuinua uchumi wa nchi. “Uzinduzi wa mafunzo ya mbinu tano za kukuza ujasiriamali ni njia mojawapo sahihi itakayoleta mafanikio katika Taifa letu”, alisema Issa.

“Kigezo kikubwa kinachohitajika kuwa mshiriki wa mafunzo hayo ni kuwa na ujuzi wa ujasiriamali na kuwa na malengo endelevu ya kukua kibiashara”, alisema Issa.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez alisema ni muhimu kwa taifa lolote lenye nia ya kujiendeleza kufikia kuwa nchi ya viwanda halina budi kuwathamini na kuwaendeleza wajasiriamali wadogo na wa kati. Bw. Rodriguea alisisitiza kuwa wajasiriliamali ndio wenye nafasi kubwa ya kutoa ajira pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Naye mwanzilishi wa Taasisi ya Fursa Tanzania, Bw. Ruge Mutahaba alisema uzinduzi wa mafunzo ya mbinu tano za kukua kijisiriamali kutafungua nafasi pana kwa taasisi na watu binafsi watakaotaka kuunga mkono na kuwa sehemu ya kuendeleza mradi huu. Hii itawapa nafasi pekee ya kushirikiana na vijana wajisiriliamali kutatua changamoto zinazowakabili katika kufikia malengo yao.

 

About Alex

Check Also

index

Mtoto wa Rais Trump atajwa kugombea nafasi ya urais wa Benki ya Dunia

Ivanka Trump binti wa rais wa Marekani, Donald Trump,ni moja ya majina yanayotajwa kuwania nafasi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

12 − eleven =