Monday , January 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / TAREHE RASMI YA KUANZA KWA MKUTANO WA KIMATAIFA WA OYES 2017 YAJULIKANA.

TAREHE RASMI YA KUANZA KWA MKUTANO WA KIMATAIFA WA OYES 2017 YAJULIKANA.

Tarehe rasmi ya kuanza kwa mkutano mkubwa wa kitaifa na kimataifa wa OYES (Open your Eyes and See) 2017 unaoandaliwa kila mwaka na kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza imejulikana.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, amebainisha kwamba mkutano huo utaanza jumamosi Mei 27 na kufikia tamati jumapili Juni 04, 2017 katika viunga vya kanisa hilo vilivyopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza.

Kupitia BMG Habari, Dkt.Kulola amebainisha kwamba waimbaji na watumishi wa Mungu kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo Mchungaji Gary White kutoka Amerika watahudumu katika mkutano huo.

Mafundisho pamoja na mahubiri ya neno la Mungu yaliyolenga kumfungua kila mmoja ili aone Ukuu wa Mungu yatafundishwa katika mkutano huo na kama ilivyo kawaida mamia ya wananchi wanatarajiwa kufunguliwa kwenye mkutano wa OYES 2017.

About Alex

Check Also

01

WAKURUGENZI NA WAGANGA WAKUU WA HOSPITALI ZA SERIKALI JIONGEZENI BADALA YA KULALAMIKA TU

Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five × two =