Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / SMZ YATILIANA SAINI NA MAKAMPUNI YA BAKHRESA KUJENGA “SERTILITE CITY” ZANZIBAR

SMZ YATILIANA SAINI NA MAKAMPUNI YA BAKHRESA KUJENGA “SERTILITE CITY” ZANZIBAR

unnamed
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega uchumi Zanzibar (ZIPA), Salum Khamis Nasor kushoto akisaini  Mkataba wa Ujenzi wa SERTILITE CITY ni  kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kulia ni Mwenyekiti wa Makapuni ya Bakhresa, Said Salim Bakhresa akisaini kwa niaba ya Makampuni hayo.
A
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega uchumi Zanzibar (ZIPA), Salum Khamis Nasor kushoto na Mwenyekiti wa Makapuni ya Bakhresa, Said Salim Bakhresa wakikabidhiana hati za Mkataba wa Ujenzi wa SERTILITE CITY mara baada ya kusaini katika hafla iliyofanyika Fumba nje kidogo ya mji wa Zanzibar 
A 1
 Picha ya pamoja ya hafla ya utiaji Saini Mkataba wa ujenzi wa Miundombinu ya Mji wa kisasa maarufu kama “SERTILITE CITY” utakaojengwa huko Fumba nje kidogo ya Mji wa Zanzibar 
unnamed
Baadhi ya Nyumba zinazoendelea kujengwa katika Mji wa kisasa maarufu kama “SERTILITE CITY” huko Fumba nje kidogo ya Mji wa Zanzibar chini ya Makapuni ya Bakhresa .
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 
………………
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 24.04.2017
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini Mkataba na Makapuni ya Bakhresa kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ya Mji wa kisasa maarufu kama “SERTILITE CITY” utakaojengwa huko Fumba nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Chini ya Mkataba huo Makampuni ya Bakhresa yatajenga Mji wa kisasa utakaobadili haiba ya nchi ambapo kukamilika kwake kutaiwezesha Zanzibar kuwa na Majengo makubwa yenye Goghofa zaidi ya 30 na Hotel zenye hadhi zaidi ya Nyota tano.
Waliotia Saini Mkataba wa Ujenzi wa “SERTILITE CITY” ni  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega uchumi Zanzibar (ZIPA), Salum Khamis Nassor kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Makapuni hayo Said Salim Bakhresa kwa niaba ya Makampuni hayo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa ZIPA Nassor ameeleza kuwa jumla ya Hekta 3,000 zimetolewa na Serikali ili kufanikisha mradi huo ambao tayari majengo kadhaa yameanza kujengwa.
Amefahamisha kuwa katika Mji huo kutakuwa na Nyumba za kibiashara za kuishi watu,zenye ukubwa tofauti kulingana na mitaa ambapo mitaa mingine zitafikia ukubwa wa zaidi ya Ghorofa 30.
“Kutakuwa na majengo tofauti kulingana na Maeneo, kutakuwa na Private Villa na katika high street kutakuwa na ghorofa zaidi ya 30” alifafanua Mkurugenzi Salum
Ameongeza kuwa kutakuwa na Kiwanja cha kimatifa cha Mpira wa Miguu na Viwanja vidogo vidogo, Kituo cha Kibiashara, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano na Bandari ndogo itakayounganisha Dar es Salaam na Pemba.
Kwa kweli itakuwa ni Mji wa kivutio wa aina yake kwa Wenyeji na Wageni mbalimbali ambao bila shaka watakuwa na shauku ya kutembelea na kupata huduma mbalimbali” alisema Mkurugenzi ZIPA. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makampuni ya Bakhresa Salim Ali Salim amesema tayari wametenga kiasi cha Dola Million 500 kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ya “Sertilite City” katika hatua za awali huku gharama ikitarajiwa kuongezeka kulingana na mahitaji ya baadae.
Aidha ameeleza kuwa manufaa yatakayopatikana ni pamoja na nafasi za ajira 3,000 za moja kwa moja kwa Wananchi jambo ambalo pia litabadili hali zao za kimaisha.
Awali Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt Khalid Salum Mohammed amewahakikishia Mashirikiano ya kila aina Wawekezaji hao Wazalendo na kuwaomba waendelee kuiunga Mkono Serikali katika azma yake ya kuwaletea maendeleo Wananchi.
Amesema Sheria Namba 11 ya Mwaka 2004 inatoa nafasi kwa Serikali kuwalinda wawekezaji hasa Wazawa na hivyo kuwaomba Wawekezaji wengine kuitumia Fursa Hiyo ili kuendelea kuwekeza zaidi Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega uchumi Zanzibar (ZIPA) imeweka mazingira salama ya kiuwekezaji hasa katika maeneo huru yaliyotengwa ili Wawekezaji Wazawa na Wageni waendelee kuwekeza katika maeneo hayo kwa ajili ya kuleta maendeleo.
Mradi huo wa Ujenzi wa Mji wa kisasa maarufu kama “SERTILITE CITY” huko Fumba utakuwa ni miongoni mwa miradi mikubwa iliyowekezwa Zanzibar na Bakhresa ambayo itaendelea kuisaidia Serikali ya Zanzibar kukuza kipato cha wananchi wake na Pato la Taifa kwa ujumla.

About Alex

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 − 4 =