Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO

VYA HABARI LEO TAREHE 24.05.2017

  • MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA ZA SHILINGI ELFU KUMI 20, ZENYE JUMLA YA THAMANI YA TSH.200, 000/=, WILAYANI NYAMAGANA.

  • WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA MICHE 37 YA BHANGI PAMOJA NA POMBE YA MOSHI (GONGO) LITA 41 WILAYANI ILEMELA.

KWAMBA TAREHE 24.05.2017 MAJIRA YA SAA 00:30HRS USIKU MAENEO YA ITALIAN PUB KATA YA IGOMA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, DEUS MARWA MIAKA 29, MKAZI WA BUSENGA, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA ZA ELFU KUMI ISHIRINI (20) ZENYE THAMANI YA JUMLA YA TSHS 200,000/=, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.

AWALI ASKARI WAKIWA DORIA MAENEO TAJWA HAPO JUU WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA WASIRI KWAMBA KATIKA MAENEO YA ITALIAN PUB ILIOPO IGOMA YUPO MTU MWENYE NOTI BANDIA. ASKARI WALIFANYA UPELELEZI NA UFUATILIAJI JUU YA TAARIFA HIZO KATIKA MAENEO HAYO, NDIPO MAJIRA TAJWA HAPO JUU  WALIWEZA KUMKAMATA MTUHUMIWA.

AIDHA BAADA YA KUKAMATWA MTUHUMIWA ALIFANYIWA UPEKUZI NA ASKARI NA KUPATIKANA AKIWA NA NOTI BANDIA ZA ELFU KUMI ISHIRINI (20) ZENYE THAMANI YA JUMLA YA  TSH 200,000/=. POLISI WAPO KATIKA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMDE MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI VIJANA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUTENGENEZA NOTI BANDIA KWANI NI KOSA LA JINAI, NA YEYOTE ATAKAYE PATIKANA WA AINA KAMA HII ATAFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA ILI HATAU STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.

KATIKA TUKIO LA PILI;

MNAMO TAREHE 23.05.2017 MAJIRA YA SAA 14:30HRS MCHANA KATIKA MAENEO YA MTAA WA SANGABUYE KATA YA SANGABUYE WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI WANAOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.JAMES KASWA MIAKA 59, MKAZI WA SANGABUYE, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA MICHE 37 YA BHANGI, ALIYOIPANDA SHAMBANI KWAKE PAMOJA NA MAZAO MENGINE NA 2.ASIA CHARLES MIAKA 32, MKAZI WA ILAGALAGALA, HUYU ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA AKIWA NA POMBE AINA YA MOSHI (GONGO) KIASI CHA LITA 41, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

AWALI ASKARI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA MAENEO TAJWA HAPO JUU WAPO BAADHI YA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI (GONGO) PAMOJA NA KILIMO CHA BHANGI, ASKARI WALIFANYA UPELELEZI KATIKA MAENEO HAYO KUHUSIANA NA TAARIFA HIZO NA BAADAE WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WAWILI TAJWA HAPO JUU.

POLISI WAPO KATIKA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WAWILI WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, AIDHA UPELELEZI NA MISAKO YA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA NA SHUGHULI HIYO HARAMU KATIKA MAENEO HAYO BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWAOMBA WAFANYE SHUGHULI HALALI ZA KUJIPATIA KIPATO NA SIO VINGINEVYO, KWANI ENDAPO MTU ATABAINIKA  HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.

IMETOLEWA NA:

DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

About Alex

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × one =