Thursday , November 23 2017

Home / MCHANGANYIKO / “MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI BANDARI YA TANGA WAIVA”

“MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI BANDARI YA TANGA WAIVA”

 Afisa
Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino
Kasale kulia akimueleza jambo 
Waziri wa Viwanda,Biashara na
Uwekezaji,Charles Mwijage kushoto wakati alipofungua maonyesho ya tano
ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako
Jijini Tanga.

 Mwanasheria
Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania
(TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao
ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya
biashara kimataifa.

 Afisa
Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino
Kasale akizungumza na waandishi wa habari leo

 

MRADI wa Bomba la Mafuta Mkoani Tanga umefikia kwenye hatua ya wataalamu kukagua njia
itakayopitisha miundombinu ya bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Bandari ya Tanga.
Hatua hiyo imekuja baada ya serikali ya Tanzania na Uganda kutiliana saini ya mkataba baina ya
nchi na nchi (Iga) kukamilika.
Hayo yalisemwa leo na
Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania
(TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao
ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya
biashara kimataifa.

Alisema tayari
wameshafanya maamuzi yameshakamilika wataalamu wanafanya tathimi ya udongo
katika njia ambayo bomba hilo litapita kwa taarifa ya awali njia iliyopatikana
upana mita 200 na baadae watalaamu wataipunguza mpaka
100.

Awali akizungumza kuhusiana na mradi huo, Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Augustino Kasale alisema
mradi huo utapita katika mikoa nane ya Tanzania na kuzalisha ajira 10000 za
kudumu na muda mfupi.

Alizitaja fursa ambazo zitakuwa moja kwa moja ni hutoaji huduma wakati wa ujenzi, ajira za muda
mfupi na moja kwa moja, fursa za usafirishaji ikiwemo kuufungua mkoa wa Tanga
kiuchumi.

“Hivyo hivi sasa wananchi wa mkoa wa Tanga wanapaswa kujiandaa na ujio wa Bomba la Mafura ghafi
kutoka hoima nchini Uganda hadi Mkoani Tanga “Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
 

About bukuku

Check Also

DSC_0298

UFUNGAJI WA MAFUNZO YA UDHIBITI USAMBAAJI MAFUTA BAHARINI WAFANYIKA ZANZIBAR

Injinia Mratibu wa maswala ya Mazingira Baharini kutoka ZMA Halfani Hamad Hassan kulia akitoa maelezo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fourteen − five =