Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA SEMINA KWA WASTAAFU WATARAJIWA WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA SEMINA KWA WASTAAFU WATARAJIWA WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu kabla ya
ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa
Benki Kuu jijini Mwanza

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa
Benki Kuu jijini Mwanza

 Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa
makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.

 Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa
makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.

 Baadhi ya Wadau wakifuatilia ufunguzi wa Semina kwa Wastaafu Watarajiwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha Vitabu vya PSPF kwenye kutoa elimu kwa Wanachama wa mfuko huo.
                             …………………………………………………………

Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza
waajira wasiopeleka au kuchelewesha michango ya wanachama kwenye mifuko ya
hifadhi ya jamii nchini wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia hiyo.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo 3-June-2017 Jijini
Mwanza wakati anafungua semina ya maisha baada ya kustaafu,fursa ya
mafao,uwekezaji iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
kwa ajili ya wastaafu watarajiwa 450 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza.
Makamu wa
Rais amesisitiza kuwa waajiri wakichangia kwa mujibu wa sheria kwenye mifuko
hiyo watawezesha wanachama wao kupata mafao kikamilifu na kwa wakati.
Kuhusu
madeni ya Serikali kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini, Makamu wa Rais amewahakikishia
Wakurugenzi wa mifuko hiyo kuwa Serikali inashughulikia madeni hayo na baada ya
kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa madeni hayo basi malipo yatafanyika haraka
iwezekanavyo.
Makamu wa
Rais amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha michango ya pensheni kwa
wafanyakazi wa taasisi zinazopata ruzuku kutoka Serikalini inalipwa kwenye
mifuko hiyo kwa wakati.
Aidha,
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wastaafu watarajiwa kote
nchini waache tabia ya kukata tamaa baada ya kustaafu bali wajipange vyema na
kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo viwanda vidogo, kilimo na
biashara.
Amesema kuwa
kama wastaafu hao watawekeza katika maeneo hayo watatoa ajira kubwa kwa vijana badala
ya kutumia mafao yao kwenye matumizi yasiyo ya lazima.
“Wazee ni rasilimali na
hazina kubwa kwa taifa kama waswahili wasemavyo panapo wazee hapaharibiki jambo
hivyo basi ni matumaini yangu kuwa mfuko wa PSPF mtaendelea kufanya kazi kwa
bidii na kwa uadilifu kuhakikisha kuwa hazina hii ya wazee wetu wanapata haki
zao kwa mujihu wa sheria za nchi pale wanapohitaji huduma toka kwenu
.”Amesisitiza
Makamu wa Rais.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameonya wastaafu hao watarajiwa kupunguza matumizi
yasiyo ya lazima bali watumie fedha watakazopata katika shughuli za kiuchumi
kwa ajili ya maslahi yao ya baadaye.
Makamu wa
Rais pia amepongeza jitihada zinazofanywa na mfuko wa PSPF kwa kutoa mafunzo
kwa wastaafu watarajiwa kwa ajili ya kuwasaidia kujipanga vyema pindi watakapostaafu
utumishi wao.
Kwa upande
wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amewahakikishia
wastaafu hao watarajiwa kuwa wa mkoa wa Mwanza kuwa Serikali itaendelea
kusimamia vyema mifuko ya hifadhi ya jamii ili iweze kutoa mafao bora na kwa
wakati.

Dkt Ashatu
Kijaji pia amehimiza wastaafu hao watarajiwa kutumia vizuri mafao wanayopata
kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

About bukuku

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fourteen + 1 =