Thursday , January 17 2019

Home / MCHANGANYIKO / MBUNGE AWESO ATAJA SABABU YA WILAYA YA PANGANI KURUDI NYUMA KIUCHUMI

MBUNGE AWESO ATAJA SABABU YA WILAYA YA PANGANI KURUDI NYUMA KIUCHUMI

MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM)
Jumaa Aweso ametaja sababu kubwa iliyoifanya wilaya hiyo kurudi nyuma
kiuchumi ni kutokana na kuchelewa kuwekeza kwenye suala la elimu na
miundombinu ya barabara ambacho ni kilio cha muda mrefu.

Hivyo kuitaka jamii kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye elimu ili iwe
chachu ya kuinua maendeleo yao lakini pia serikali iboreshe miundombinu
ya barabara ya Tanga -Pangani hadi Sadaani ambayo imekuwa ikipigiwa
kelele na wabunge waliopita bila mafanikio

Aweso aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wananchi wa
Jimbo hilo ambapo alisema wazazi hawana budi kuwekeza kwenye elimu
iliwaweze kupatikana wataalamu watakaosaidia harakati za kuinua
maendeleo.

Alisema ili katika mipango mikubwa ya kufanikisha azma hiyo ndio sababu
kubwa wakaanzisha mpango mahususi wa niache nisome mwaka jana ambao
umepata mafanikio makubwa.

“Mpango wa niache nisome umekuwa mkombozi mkubwa wa kuihamasisha jamii
ya wana pangani kuona umuhimu wa kupata elimu na mafanikio
yaliyopatikana ni mengi ikiwemo kupata fursa mwaka huu kuwapeleka vijana
wengi Jeshini “Alisema

Aidha aliwataka viongozi chama na serikali kuendelea kushirikiana na
wataalamu ili kuwezesha kuifungua wilaya ya Pangani ambayo inahitaji
kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

“Uchumi wa Pangani ni zao la Mnazi na mtu mpaka aje wilayani hapa lazima
awe na sababu maalumu ikiwemo kufiwa nah ii inasababishwa na
miundombinu mibovu ya barabara hivyo ujenzi huo utakapoanza utasaidia
kufungua uchumi huo “Alisema.

Mbunge huyo aliwataka pia wananchi wa wilaya hiyo kutunza maeneo yao kwa
kuacha kuyauza ovyo kutokana na fursa kubwa inayokuja mkoani hapa
ikiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta.
 Habari kwa Hisani ya Blog
ya Kijamii ya Tanga Raha

About bukuku

Check Also

PIC 3

KAMATI YA UONGOZI YA CHAMA CHA MABUNGE NCHI WANACHAMA WAJUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA (CPA AFRICA REGION) YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  (kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Kenya Mhe. …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

three − 1 =