Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / KAULIMBIU MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 20117

KAULIMBIU MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 20117

 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KAULIMBIU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA JUNI 16, 2017

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na asasi za kiraia itaungana na mataifa mengine barani Afrika kusherehekea sikuu ya mtoto wa Afrika kwa Mwaka 2017 Kitaifa mkoani Dodoma tarehe 16 Juni mwaka huu.

Wizara inatoa taarifa kwa vyombo vya habari pamoja na wadau wengine kuwa, Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka huu 2017 ni “Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa sawa kwa Watoto”.

 

Wizara inatoa wito kwa  vyombo vya habari waandishi wa habari kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika kuelimisha jamii kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu ambayo inahimiza uzingatiaji wa jukumu la ulinzi na usalama wa Mtoto na utoaji wa haki sawa kwa watoto wote ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo mwaka 2030.

 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)

06/6/2017

About Alex

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 + one =