Monday , December 10 2018

Home / MICHEZO / SIMBA SC UWANJANI LEO MICHUANO YA SPORTPESA!

SIMBA SC UWANJANI LEO MICHUANO YA SPORTPESA!

Washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Simba leo wanatupa kete yao ya kwanza kwenye michuano ya SportPesa Super Cup watakapomenyana na Nakuru All Stars Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam

Mchezo huo utaanza Saa 8:00 mchana na utafuatiwa na mchezo wa pili wa kundi hilo, baina ya Jang’ombe Boys ya Zanzibar na Gor Mahia ya Kenya hapo hapo Uhuru.
Michuano hiyo ilianza jana Uwanja wa Uhuru, mabingwa wa Tanzania wakiwang’oa mabingwa wa Kenya, Tusker FC kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Awali ya hapo, vigogo wa Kenya, AFC Leopards nao waliitupa nje Singida United kwa penalty 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 pia.
Bingwa wa michuano hii atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 30,000 zaidi ya Sh. Milioni 65 za Tanzania pamoja na nafasi ya kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Everton ya England

RATIBA NA MATOKEO SPORTPESA SUPER CUP
Juni 5, 2017
Singida United 1-1 AFC Leopards (Penalti 4-5)
Yanga SC 0-0 Tusker FC (Penalti 4-2)
Juni 6, 2017
Jang`ombe Boys vs Gor Mahia
Simba Vs Nakuru All Star
NUSU FAINALI
Juni 8, 2017
AFC Leopards Vs Yanga SC
Simba SC/Nakuru All Star Vs Jangombe Boys/Gor Mahia
FAINALI
Juni 11, 2017

About Alex

Check Also

7178932-0-image-m-13_1544301930293

MESSI AFUNGA MABAO MAWILI BARCELONA YAICHAPA 4-0 ESPANYOL UGENINI LA LIGA

Lionel Messi akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia mabao mawili Barcelona dakika za 17 na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 × 5 =