Thursday , December 14 2017

Home / MCHANGANYIKO / BENKI YA DTB, EFM RADIO WATOA MSADA WA MADAWA TAASISI YA MIFUPA MOI

BENKI YA DTB, EFM RADIO WATOA MSADA WA MADAWA TAASISI YA MIFUPA MOI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI, Dkt.Respicious Boniface, (kulia), akipokea sehemu ya msada wa madawa kutoka kwa Meneja wa Benki ya DTB Tawi la Morocco jengo la Airtel, jijini Dar es Salaam, Bi.Sheena .Y. Sinare, kwenye jengo jipya la MOI, leo Juni 18, 2017. DTB kwa kushirikiana na EFM Radio, wametoa msada wa madawa mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 4 ili kusaidia watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo
 Dkt. Boniface, akipokea sehemu ya msada wa madawa kutoka kwa Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Jesca Mwanyika kwenye jengo jipya la MOI jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2017. EFM kwa kushirikiana na Benki ya DTB wametoa msada huo wa madawa yenye thamani ya shilingi milioni 4 ili kusaidia watoto wenye matataizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo
 Mtayarishaji wa kipindi cha “Bustani ya Watoto” kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo, Bi. Flora Amon maarufu kama  Aunt FIFI, akikabidhi sehemu ya msada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Precious Boniface
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI
ya DTB kwa kushirikiana na EFM Radio kupitia kipindi chake cha “Bustani ya Watoto”, wametoa msada wa
madawa mbalimbali kwa Taasisi ya Mifupa MOT iliyoko Hospitali ya Taifa
Muhimbili jijini Dar es Salaam, leo Juni 18, 2017.
Akikabidhi
madawa hayo, Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Bi.Jesca Mwanyika alisema, EFM
kupitia kipindi chake cha watoto cha “Bustani
ya Watoto”
iliamua kuwashirikisha DTB ili kuona ni namna gani wanaweza
kusaidia watoto waliolazwa kwenye Taasisi ya MOI hususan wale wenye matatizo ya
kichwa kikubwa na mgongo wazi.
“Sisi
kama EFM Radio tuna kipindi cha watoto cha Bustani ya Watoto, tumeona kwa vile
tunashughulika na watoto, na kwa vile siku chache zilizopita Dunia iliadhimisha
siku ya mtoto wa Afrika Duniani, basi tumeona tutoe kiasi hiki cha madawa
kuwasaidia watoto hawa wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi
waliolazwa hapa MOI.”Alisema Bi. Jesca.
Akizungumza
kwa niaba ya DTB, Afisa Masoko wa benki hiyo, Bw.Baguma Ambari alisema, Benki
kama taasisi inayotoa huduma kwa wananchi, inao wajibu mkubwa kutoa sehemu ya
faida yake kusaidia jamii na hivyo imefurahishwa kuungana na EFM Radio katika
kutoa msada huo wa madawa ambao anaamini utasaidia katika kuwahudumia watoto
hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Akitoa
shukrani zake, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface alisema,
msada huo wa madawa utasaidia sana katika kuwapatia huduma za afyan watoto hao.
“Kama mjuavyo wengi wa watoto hawa hutoka kwenye familia masikini kwa hivyo
msada huu wa madawa utasaidia sana katika kuwapatia huduma
“Madawa
haya ni anti-biotic pamoja na kwamba watoto hawa wanaletwa hapa wakiwa na
matatizo ya vichwa  baadhi yao huwa na
infection sehemu mbalimbali za miili kama vile vifua au tumboni, lakini pia
husaidia kutibu vidonda n.k.” Alifafanua Dkt. Boniface.

 

 Dkt. Boniface (mbele) akiongozana na Meneja wa DTB Tawi la Morocco jijini Dar es Salaam, Bi.Sheena Y. Sinare, wakati wakitembelea kuwajulia hali watoto hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa kwenye taasisi ya mifupa MOI jijini Dar es Salaam
 Dkt. Boniface (kushoto), akizungumza jambo na Bi. Sinare wakati walipokuwa kwenye moja ya wodi za watoto hao

Dkt. Boniface (kushoto), akizungumza jambo na Bi. Sinare wakati walipokuwa kwenye moja ya wodi za watoto hao kuwajulia hali

 Afisa Masoko wa DTB, Bw. Baguma Ambar(kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kutoa msada huo. Kulia ni Kaimu Afisa Uhusiano wa MOI, Bw.Frank Matua
 Afisa Masoko wa DTB, Bw. Baguma Ambar, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kutoa msada huo.
  Mtayarishaji wa kipindi cha “Bustani ya Watoto”
kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo,
Bi. Flora Amon maarufu kama  Aunt FIFI,akielezea kilichomsukuma kuwa na mpango huo wa kutoa msada
   Mtayarishaji wa kipindi cha “Bustani ya Watoto”
kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo,
Bi. Flora Amon maarufu kama  Aunt FIFI,akielezea kilichomsukuma kuwa na mpango huo wa kutoa msada. Kulia anayesikiliza kwa makini, niAfisa Uhusiano wa EFM, Bi. Jesca Mwanyika
 Dkt. Boniface akitoa neno la shukurani baada ya kupokea msada huo
  Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface akitoa neno la shukurani baada ya kupokea msada huo
 Baadhi ya wafanyakazi wa EFM na DTB waliohudhuria hafla hiyo
  Baadhi ya wafanyakazi wa EFM  waliohudhuria hafla hiyo
 Mfanyakazi wa EFM, Bw.Sali Mlindila, akiwa amebeba boksi lenye dawa zilizotolewa msada kwa MOI
Wafanyakazi wa EFM na DTB wakisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface alipokuwa akielezea umuhimu wa jamii kuwasaidia watoto hao.
Wafanyaakzi wa EFM na watoto wao na wale wa DTB wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface

About bukuku

Check Also

P_20171213_112357_vHDR_On-1

RC Wangabo asimamisha shughuli za uvuvi Ziwa Rukwa Kujikinga na Kipindupindu.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilanga, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × 5 =