Thursday , December 14 2017

Home / MCHANGANYIKO / Muhimbili Yamtia Mbaroni Daktari Feki Leo

Muhimbili Yamtia Mbaroni Daktari Feki Leo

DK FEKI

Kulia ni daktari feki ambaye amekuwa akijitambulisha kwamba ni Dk Abdallah Juma ambaye amekuwa akifanya kazi katika Maabara Kuu, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni mmoja wa askari wa Muhimbili aliyemkamata daktari huyo.

………………………………………………………………………

 Hospitali  ya Taifa Muhimbili (MNH) imemtia mbaroni kijana mmoja aliyekuwa akijifanya daktari na alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwamba anaitwa Dk Abdallah Juma.
Mtu huyo alikuwa akijifanya kutoa huduma katika Maabara Kuu. Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa kijana huyo ni daktari feki na si daktari kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo.
Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa walinzi walikuwa wakimtilia shaka na kuanza kumfuatilia hadi walipofanikiwa kumkamata.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni madaktari kama huyo ambaye amekamatwa leo.

About bukuku

Check Also

P_20171213_112357_vHDR_On-1

RC Wangabo asimamisha shughuli za uvuvi Ziwa Rukwa Kujikinga na Kipindupindu.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilanga, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five × five =