Tuesday , September 25 2018

Home / BIASHARA / WAZIRI WA ARDHI MH. WILLIAM LUKUVI ATEMBELEA BANDA LA (WHC) KATIKA MAONYESHO YA SABASABA LEO

WAZIRI WA ARDHI MH. WILLIAM LUKUVI ATEMBELEA BANDA LA (WHC) KATIKA MAONYESHO YA SABASABA LEO

1

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya nyumba za watumishi (WHC) Dk. Fred Msemwa wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo leo kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea katika  viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke jijini Dar es salaam, Katikati ni Afisa Masoko na Uhusiano wa (WHC)Bi. Maryjane Makawia.

Mara baada ya kutembelea banda hilo Waziri Lukuvi amewaambia waandishi wa habari kwamba serikali haitaondoa (VAT) katika vifaa vya ujenzi hivyo taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na ujenzi wa nyumba zinatakiwa kujipanga na kuchukua hatua mbalimbali za kupunguza gharama za ujenzi wa miradi yao ikiwa ni pamoja na kutumia teknolojia rahisi na ya kisasa  isiyochukua gharama kubwa katika ujenzi wa nyumba.

2

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya nyumba za watumishi( WHC) Dk. Fred Msemwa  katikati wakati  wakati alipotembelea katika banda hilo leo,  kushoto ni Afisa Mauzo (WHC) Bi. Irene Kasanda na wa pili kutoka kulia ni Afisa Masoko na Uhusiano wa (WHC) Bi. Maryjane Makawia.

3

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya nyumba za watumishi (WHC) Dk. Fred Msemwa wakati alipokuwa akifafanua mambo kadhaa  kwa waziri  alipotembelea katika banda lao.

4

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda hilo.

5 6

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya nyumba za watumishi (WHC) Dk. Fred Msemwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Mh. Waziri William Lukuvi kuwatembelea katika banda lao kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano wa (WHC)Bi. Maryjane Makawia.

7

Afisa Mauzo (WHC) Bi. Irene Kasanda  kushoto  na  Afisa Masoko na Uhusiano (WHC) Bi. Maryjane Makawia wakipozi kwa picha.

8

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya nyumba za watumishi (WHC) Dk. Fred Msemwa akizungumza na mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda la taasisi hiyo.

About bukuku

Check Also

MADENI PIC 1

MDAIWA SUGU  WA USHURU JIJI LA ARUSHA ANASWA

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni  akiwa ndani ya duka la mmoja wa wafanyabiashara …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

three × 2 =