Monday , October 22 2018

Home / MICHEZO / ARSENAL YAANZA KUNYAKUWA MAKOMBE,YAITANDIKA CHELSEA NA KUBEBA NGAO YA JAMII

ARSENAL YAANZA KUNYAKUWA MAKOMBE,YAITANDIKA CHELSEA NA KUBEBA NGAO YA JAMII

4304DB2E00000578-4765490-Arsenal_won_the_first_trophy_of_the_2017_18_season_against_Chels-m-304_1502033031205
Mabingwa watetezi wa Kombe la FA CUP timu ya Arsenal imenyakuwa kombe la Ngao ya Hisani baada ya kuwalaza Chelsea kwa jumla ya Penalti 4-1 kutokana na dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa pande zote mbili baada ya milango yote kushindwa kufungana huku Arsenal wakipata pigo baada ya Nahodha Per Mertesacker aliyechanika kwenye uso wake wa jicho baada ya kugongana na Cahil wakati wakiruka juu na nafasi yake kuchukuliwa na Kolasinac.
5
Kipindi cha pili kilianza kwa Chelsea kupata bao dakika ya 48 likifungwa na mchezaji wa Nigeria Moses
4
Kunako dakika ya 84 kiungo mshambuliaji wa Chelsea Pedro kuoneshwa kadi nyekundu moja kwa moja baada ya kumchezea vibaya Elneny na Xhaka kupiga faulo na kumkuta beki wa pembeni Kolasinac kusawazisha kwa kichwa hadi dakika 90 timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na kupelekea kwenda matuta.
3
2
Wachezaji walioweza kupata Penalti kwa upande wa Arsenal ni Walcott,Monreal,Oxlade-Chamberlain na Giroud huku Chelsea bao lao likifungwa na Cahill,huku Courtois na Morata wakikosa
VIKOSI VILIVYOANZA:
Arsenal: Cech, Holding, Mertesacker, Monreal, Bellerin, Elneny, Xhaka, Oxlade-Chamberlain, Welbeck, Iwobi, Lacazette.
Subs: Giroud, Ospina, Walcott, Maitland-Niles, Kolasinac, Nelson, Joseph Willock.
 
Chelsea: Courtois, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Moses, Fabregas, Kante, Alonso, Willian, Pedro, Batshuayi.
Subs: Caballero, Rudiger, Morata, Musonda, Christensen, Scott, Boga.

About Alex

Check Also

Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na wasanii mbalimbali waliojitokeza kwenye maziko ya msanii mwezao Mashaka jana.

RIDHIWANI KIKWETE AUNGANA NA WASANII KUMZIKA MASHAKA

Na Shushu Joel,Dar MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 + 4 =