Monday , December 10 2018

Home / MICHEZO / AVEVA NA KABURU WARUDISHWA RUMANDE HADI AGOSTI 16

AVEVA NA KABURU WARUDISHWA RUMANDE HADI AGOSTI 16

AVEVA-NA-KABURU-640x320
Kesi inayowakabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange Kaburu imesogezwa mbele hadi Agosti 16, mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.
Aveva na Kaburu, wamerudishwa tena rumande katika gereza la Keko jijini Dar es Salaam.
Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesi hiyo ilitajwa kwa mara ya tano mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambaka. Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za klabu hiyo na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya 650 Milioni) na wamekuwa rumande tangu Juni 29 mwaka huu.
Katika kesi hiyo upande wa mashitaka uliongozwa na wakili wa mwandamizi wa Serikali, Leonard Chalo na Kishemi Mutalemwa, waliomba wapangiwe tarehe nyingine kwa kuwa upelelezi haujakamilika.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambaka aliliridhia ombi la mawakili wa serikali huku akiwataka kukamilisha upelelezi huo.
Kufuatia ombi hilo lililotolewa, mawakili wa upande wa utetezi, Philemon Mutakyamirwa na Evodius Mtawala waliiomba mahakama hiyo kesi itajwe tena Agosti 16, mwaka huu.

About Alex

Check Also

7178932-0-image-m-13_1544301930293

MESSI AFUNGA MABAO MAWILI BARCELONA YAICHAPA 4-0 ESPANYOL UGENINI LA LIGA

Lionel Messi akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia mabao mawili Barcelona dakika za 17 na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

one × three =