Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / JWTZ Wapokea Vifaa Vya Michezo Kutoka NMB

JWTZ Wapokea Vifaa Vya Michezo Kutoka NMB

unnamed

Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB – Boma Raballa (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) – Kanali Richard Mwandike (kulia) leo jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi, mipira na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 10, vitatumiwa na wachezaji wa timu ya JWTZ wanaotarajia kusjiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017.
Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) – Kanali Richard Mwandike (kulia) akimshukuru Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB – Boma Raballa (kushoto) mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo leo jijini Dar es Salaam vilivyotolewa na NMB kuwezesha timu ya JWTZ kushiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017.
Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB – Boma Raballa (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) – Kanali Richard Mwandike (kulia) leo jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi, mipira na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 10, vitatumiwa na wachezaji wa timu ya JWTZ wanaotarajia kusjiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017.

Na Mwandishi Wetu,

BENKI ya NMB leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) inayotarajia kushiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki itakayofanyika jijini Bujumbura – Burundi. Vifaa vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na mipira kwaajili ya timu ya mpira wa miguu, mipira ya mchezo wa mikono (wasichana) na mipira mchezo wa kikapu kwa wanaume (Basket ball).

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa JWTZ – Kanali Richard Mwandike, Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB – Boma Raballa alisema vifaa vingine ni pamoja na mipira 10 ya mchezo wa volebo (Volleyball), jezi 42 za mpira wa miguu, seti mbili za jezi mpira wa kikapu (wasichana), seti mbili za jezi mpira wa basket na seti mbili za jezi mpira wa Volleyball.

Vifaa vingine vilivyokabidhiwa ni pamoja na seti mbili za jezi za waamuzi kwa michezo ya Netball, Basketball, Volleyball na mabegi 30 ya wachezaji ambapo vyote kwa ujumla vina thamani ya shilingi milioni 10 za Kitanzania.

Bw. Raballa alisema kuwa msaada huo umetokana na ushirikiano mzuri na wa muda mrefu kati ya benki ya NMB na jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na ndiyo maana wakaona umuhimu wa kuendelea kuwashika Mkono kupitia msaada kwa timu za jeshi zinazoenda kushiriki mashindano ya majeshi ya jumuia ya afrika ya mashariki.

“…Hii si mara ya kwanza kusaidia katika mashindano haya, kwani nakumbuka hata mwaka jana tuliwasaidia baadhi ya vifaa vya michezo kushiriki katika mashindano haya. Tunaamini vifaa hivi mbali na kuendeleza ushirikiano wetu mzuri, vitakuwa chachu ya kufanya vizuri katika mashindano haya muhimu kwa jumuia ya Afrika ya Mashariki,” alisema Raballa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa JWTZ – Kanali Richard Mwandike akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya JWTZ alisema anaishukuru NMB kwa msaada wa vifaa hivyo na kuongeza kuwa msaada huo umewapa morali ya kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano hayo.

Kanali Mwandike aliongeza kuwa timu hiyo itatumia jezi na vifaa vingine walivyo kabidhiwa kwenye mashindano hayo huku wakiahidi kuwa mabalozi wazuri wa NMB nan chi kwa ujumla. Kwa Mwaka wa 6 mfululizo, NMB imekuwa ikisaidia timu za Majeshi wanapoenda kuwakilisha nchi kupitia michezo mbalimbali na katika mashindano mbalimbali.

Meneja Mahusiano Kitengo cha Mikopo NMB, Emmanuel Mahodanga (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) – Kanali Richard Mwandike (kulia) katika hafla hiyo.
Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB – Boma Raballa (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) – Kanali Richard Mwandike (kulia) leo jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi, mipira na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 10, vitatumiwa na wachezaji wa timu ya JWTZ wanaotarajia kusjiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017.

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × 5 =