Tuesday , December 11 2018

Home / MICHEZO / KLABU YA SIMBA YATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) NA KUKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI MBILI KWA AJILI YA MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO KWA MTOTO MWAMVITA HASSAN

KLABU YA SIMBA YATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) NA KUKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI MBILI KWA AJILI YA MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO KWA MTOTO MWAMVITA HASSAN

Simba 1

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza umuhimu  wa mchezaji kupima magonjwa ya moyo ili kuepuka  kupata madhara ya ugonjwa huo wawapo uwanjani kwa baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu ya Simba waliotembelea Taasisi hiyo leo.

Simba 2

Nahodha wa timu ya Simba Method Mwanjali akimkabidhi hundi ya shilingi milioni mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo za mtoto Mwamvita Hassan (wa pili kulia) ambaye anatibiwa katika Taasisi hiyo. Kulia ni Msemaji wa timu ya Simba Haji Manara.

Simba 3

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi pamoja na wachezaji wa timu ya Simba mara baada ya kumaliza ziara yao ya kuitembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Simba 4

Wachezaji wa timu ya Simba Haruna Niyonzima na Nicholaus Gyan walimsikiliza  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alipokuwa aliwaeleza madhara yatokanayo na magonjwa ya Moyo anayoweza kuyapata mchezaji awapo uwanjani. Baadhi ya viongozi wa timu hiyo pamoja na wachezaji walitembelea JKCI leo kwa ajili ya kuona huduma wanazozitoa pamoja na kukabidhi hundi ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa mtoto Mwamvita Hassan.

Simba 5

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na mchezaji wa Timu ya Simba Haruna Niyonzima mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Taasisi hiyo leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Simba Dkt. Anord Kashembe.

Simba 6

Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Godwin Sharau akiwaeleza wachezaji wa timu ya Simba aina mbalimbali za upasuaji wa moyo kwa watoto wanazozifanya wakati baadhi ya wachezaji wa timu hiyo pamoja na viongozi  walipotembelea Taasisi hiyo leo.

Simba 7

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu ya Simba na mtoto  Mwamvita Hassan ambaye timu hiyo imemlipia shilingi milioni mbili kwa ajili ya gharama za upasuaji wa Moyo.

Simba 8

Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya Simba waliotembelea Taasisi hiyo leo.

Picha na JKCI

About Alex

Check Also

7212630-6477327-image-m-19_1544394932492

RIVER PLATE WAIPIGA BOCA JUNIORS NA KUBEBA COPA LIBERTADORES

Wachezaji wa River Plate wakifurahia na taji lao la Copa Libertadores baada ya ushindi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

15 − 14 =