Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / WADAU WA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL WAMPONGEZA WAZIRI MAGHEMBE

WADAU WA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL WAMPONGEZA WAZIRI MAGHEMBE

1 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Wadau wa Shamba la Miti wa Sao Hill katika kikao kilichofanyika jana mjini Mafinga Mkoani Iringa2

Baadhi ya Wadau wa Shamba la Miti wa Sao Hill wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe katika mkutano uliofanyika mjini Mafinga mkoani Iringa
……………………..

Wadau wa Shamba la miti la Sao Hill wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe kwa utaratibu mzuri wa ugawaji wa malighafi ya miti kwa kuwa umesaidia kuwaondoa madalali waliokuwa wanapewa mgawo na kisha wao kuwauzia wenye viwanda kwa bei ya juu.

Wadau hao wamebainisha hilo jana wakati  Waziri Maghembe  alipokutana nao katika ziara aliyoifanya  katika Shamba la miti la Sao Hill  lililoko wilayani Mufindi ,mkoani Iringa.

Waziri Maghembe alisema kuwa ugawaji wa malighafi ya miti kwa mwaka huu umefanywa kwenye wenye viwanda tu ili kuhakikisha wanakuwa na malighafi ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza viwanda

Aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda hivyo wadau hao wasiishie kupasua mbao pekee wahakikishe wanatengeneza bidhaa kama vile samani katika viwanda vyao.

Alisema lengo la Serikali siyo kuishia kugawa malighafi ya miti na kupasua mbao, bali ni kutengeneza  viwanda vya mazao ya mbao

Katika hatua nyingine, Waziri Maghembe amewaagiza wadau  wanaotumisa misumeno aina ya Ding dong kuacha mara moja kwa ina ufanisi hafifu na zinapoteza kiasi kikubwa cha magogo badaala yake waanze kutumia za kisasa.

Aidha, Waziri Maghembe amepunguza bei ya  miti aina mikaratusi kuanzia mwaka ambapo ada ya tozo za barabara imepunguzwa kutoka shilingi 35,000 hadi shilingi 17,8000, hatua hiyo inakuja mara baada ya wadau kumuomba Maghembe aweze kupunguza bei ya miti hiyo.

Wakati huo huo Waziri Maghembe amepiga marufuku kwa wanavijiji waojaribu kumega eneo la msitu kwa ajili ya shughuli nyingine

 

‘’Hakuna kipande chochote cha ardhi katika shamba hili kitakachochukuliwa kwa ajili ya shughuli nje ya hii inayofanyika kwa sasa’’ alisisitiza Maghembe.

 

Alisisitiza vijiji viendelee kupata fedha za mgawo wa miti ili watumie kwa shughuli za maendeleo.

 

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema kuwa utaratibu uliotumika mwaka huu wa ugawaji wa malighafi umekuwa mwarobaini wa kupunguza malalamiko kwa wadau ukilinganisha na miaka iliyopita

Aidha, aliawapongeza wafanyabiashara na wadau wa shamaba hilo kwa kulipa kodi stahiki za Serikali

 

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × two =