Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / WAZIRI WA KILIMO ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA MAONYESHO NIDA MKOANI LINDI NA KUSISITIZA KUANZA KWA MATUMIZI YA VITAMBULISHO VYA TAIFA

WAZIRI WA KILIMO ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA MAONYESHO NIDA MKOANI LINDI NA KUSISITIZA KUANZA KWA MATUMIZI YA VITAMBULISHO VYA TAIFA

IMG_6129

Baadhi ya wananchi wakishuhudia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Bw. Omary R. Ntungu akiweka saini kwenye Kitabu cha wageni alipofika kwenye banda la NIDA kushuhudia usajili unaoendelea kwa wananchi.

IMG_6132

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hamad  Rashid Mohamed akiweka saini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika maonyesho ya Kilimo Nanenane viwanja vya Ngongo – Lindi.

IMG_6149

Mhe. Hamad  Rashid Mohamed akifafanua jambo kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIDA Bi. Rose Mdami akiwa kwenye banda la NIDA kukagua shughuli za Usajili zinazoendelea kwa wananchi wa mkoa wa Lindi na Mtwara.

IMG_6163

Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hamad  Rashid Mohamed akipokea taarifa ya utekelezaji zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIDA Bi. Rose Mdami wakatI Waziri huyo alipotembelea Banda la NIDA kwenye viwanja vya Ngongo Lindi.

IMG_6164

Mhe. Hamad  Rashid Mohamed akiagana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIDA Bi. Rose Mdami baada ya kuhitimisha ziara yake katika Banda la NIDA.

IMG_6167

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi akiweka saini kwenye kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonyesho la NIDA. Kushoto ni Mhe. Aziza A. Mangosongo Mkuu wa Wilaya ya Newala.

IMG_6186

Mhe. Zambi akiteta jambo na Afisa Uhamiaji Ndugu Kudrack Edward Kuvugwa na Afisa wa NIDA, na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Newala Bi.Aziza (Katikati)

IMG_6197

Wananchi wakisuburi huduma kwenye Banda la Mamlaka ya Vitambulisho Ngongo- Lindi wakati wa maonyesho ya sherehe za Kilimo Nanenane.

IMG_6207

Afisa Usajili NIDA Bw. Praygod Mndeme akisimamia ujazaji wa fomu ya mmoja wa wananchi wakazi wa Kata ya Jamhuri mtaa wa Tulieni mkoani wa Lindi.

IMG_6211

Afisa wa NIDA Bw. Godfrey Simon Mayala akitoa ufafanuzi wa wananchi waliofika kupata huduma kwenye banda la NIDA.

………………………………………………………………………

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohamed ametembelea Banda la Maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya (NIDA) na kushuhudia umati wa wananchi waliojitokeza kusajiliwa, wakiendelea na hatua za Usajili na Utambuzi katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi ambako maonyesho hayo yanafanyika.

Kisha kupokea taarifa fupi ya utendaji kwenye Banda Hilo, Waziri huyo amepongeza kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa – NIDA katika kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa na kuitaka NIDA kuharakisha zoezi hilo kwani mahitaji ya Vitambulisho vya Taifa kwa sasa ni makubwa kutokana na matumizi mapana ya vitambulisho hivyo katika kufikia uchumi wa kati.

“ Nawapongeza wananchi wote waliojitokeza, hii inaonyesha uelewa mkubwa walionao wananchi wa kuwa na Vitambulisho vya Taifa. Ni wakati sasa wa kuongeza wigo wa matumizi ya Vitambulisho na kuwezesha Taasisi za Serikali kubadilishana taarifa kama yalivyo malengo ya kuanzishwa kwa mfumo huu” alisisitiza.

Viongozi wengine waliotembelea Banda la NIDA leo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi ambaye aliambatana na Mhe. Aziza A. Mangosongo Mkuu wa Wilaya ya Newala.

Wengine ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi Bwana Omary R. Ntungu ambaye amefurahishwa na utulivu mkubwa wa wananchi wakati wa kupatiwa huduma ya usajili.

Kilele cha maadhimisho ya sherehe za Nanenane Kitaifa zitafanyika mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo ambapo mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Hassan Suluhu.

About bukuku

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

six + thirteen =