Thursday , December 14 2017

Home / MCHANGANYIKO / KIONGOZI WA MBIO MWENGE KITAIFA AMWAGIZA MKANDARASI KUFANYA MAREKEBISHO SOKO LA NAFAKA LA NAMONGE

KIONGOZI WA MBIO MWENGE KITAIFA AMWAGIZA MKANDARASI KUFANYA MAREKEBISHO SOKO LA NAFAKA LA NAMONGE

Wakimbiza mwenge Kitaifa wakikagua Soko la Namonge.

 

Soko la Mazao la Namonge

 

Kiongozi wa mbio za mwenge akikagua baadhi ya mabanda kwenye Soko la nafaka la Namonge.

 

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga akionesha  eneo la ukuta wa Ghara kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.

 

 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Amour Hamad Amour akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri ya Bukombe Chacha Moseti.

 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Amour Hamad Amour Akizindua  Soko la Mazao baada ya kuwa ametoa maelekezo ya ukarabati wa soko hilo.

PICHA NA JOEL MADUKA(MADUKA ONLINE)

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;}

 

Kiongozi wa
mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour
Hamad  Amour  amesikitishwa na Ujenzi wa mradi  wa soko la Mazao Namonge   lililopo  wilayani Bukombe  Mkoani Geita  kwa kujengwa chini ya kiwango na hali ambayo
imepelekea kuwepo kwa nyufa nyingi kwenye maeneo mengi ya jingo hilo.


Na pia  amemtaka mkandarasi kurekebisha haraka
iwezekanavyo kabla ya mwenge wa uhuru kuondoka Mkoani humo huku akimpa siku
mbili maeneo yote ambayo yananyufa kufanyiwa ukarabati haraka zaidi.


Kiongozi
huyo wa mwenge ameendelea kuwasisitiza   viongozi
wa halmashauri kuhakikisha wakandarasi wanakuwepo katika miradi
inayozinduliwa,kuwekewa jiwe la msingi na kutembelewa na mwenge wa uhuru ili
kujibu changamoto zitokanazo na miradi hiyo.


Mhandisi wa
ujenzi wa halmashauri hiyo CHACHA MOSETI  ametoa  taarifa
ya mradi huo kwa mwenge na gharama
Sh,581,217,690 hadi kukamilika kwake ambapo Sh,552,156,805.5 ni Fedha za
serikali kuu kupitia mpango wa market insfrastructure,value addition and Rural
Finance na Sh,29,060.884.5 ni mchango wa Halmashauri.


Aidha mpaka
sasa jumla ya fedha zilizotumika ni Sh ,552,156.805.5 ambazo ni fedha za
serikali kuu.


Hata hivyo Baada
ya kukagua maeneo mbalimbali ya soko hilo  na kujionea ujenzi huo Kiongozi wa mbio za
mwenge wa uhuru kitaifa AMOUR HAMAD AMOUR akatoa maagizo.


“Baada ya
kukagua mradi huu tumeona mapungufu mengi mradi umepasuka kwenye kuta sasa kwa
vile mradi huu umekusudiwa kuwekewa jiwe la msingi na tumemuuliza mkanadarsi
hayupo eneo husika wakandarasi wanatakiwa kuwepo kwenye mradi ili kujibu
maswali ambayo yatakuwa yakiulizwa Tunamuomba mkandarasi kabla ya risala ya
utii kwa 

Mheshimiwa Rais awe amefika uwanjano na tunatoa siku mbili awe
amekamilisha ukarabati wa kasoro ambazo tumezikuta “Alisisitiza Hamad.


Wafanyabiashara
wa zao hilo Mlalu Bundala na Emmanuel Mhuli Kasuku wamezungumzia umuhimu wa
soko hilo litakapokamilika  kuwa
litawasaidia kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya zao
ambalo wanalilima.


Kauli mbiu
ya mwenge huu ni “Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi
yetu.”IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

About Alex

Check Also

P_20171213_112357_vHDR_On-1

RC Wangabo asimamisha shughuli za uvuvi Ziwa Rukwa Kujikinga na Kipindupindu.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilanga, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × 4 =