Tuesday , January 16 2018

Home / MICHEZO / Wajumbe wa Kamati Kuu ya TFF wametakiwa kuchagua viongozi waadilifu na waaminifu kuendeleza soka nchini

Wajumbe wa Kamati Kuu ya TFF wametakiwa kuchagua viongozi waadilifu na waaminifu kuendeleza soka nchini

Pix 1

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto mwenye miwani) akipokelewa na viongozi alipowasili katika Ukumbi wa St. Gasper kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) leo Mkoani Dodoma.

Pix 2

Kaimu Rais wa TFF Ndg. Wallace Karia akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu leo katika ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma

Pix 3

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) (hawapo pichani) alipokua akifungua Mkutano Mkuu wa TFF leo Mkoani Dodoma.

Pix 4

Mwakilishi kutoka CAF Bw. Souleman Hassan Waberi akitoa neno kwa wajumbe wa TFF (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) leo Mkoani Dodoma.

Pix 5

Baadhi wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wakisikiliza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo leo Mkoani Dodoma.

Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

………………………………………………………………………………

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Tarehe: 12/08/2017

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka Wajumbe wa kamati kuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwatendea haki watanzania na kuwa makini kuchagua viongozi waadilifu na waaminifu bila kuyumbishwa ama kupokea rushwa kwa ajili ya kumchagua mgombea.

Kauli hiyo ameitoa leo Mkoani Dodoma alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa TFF ambapo amewaomba wajumbe hao kuwawakilisha wadau wote wa soka nchini kwa kuwa na dhamira na uzalendo utakaowawezesha kuibua viongozi waadilifu.

“Viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wasioyumbishwa na vishawishi vya rushwa bali kuongozwa na dhamira njema na uzalendo unaozingatia ukomavu wa demokrasia tuliyonayo” amesema Mhe. Mwakyembe

Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali inataka uongozi ambao utakaoshirikiana na serikali kuendeleza michezo, kuendeleza vipaji vilivyoibuliwa kupitia michezo ya UMISETA NA UMITASHUMTA, pamoja na kuilea iliyokuwa Serengeti boys ambayo kwa sasa ni ngorongoro heros ili iiwakilishe nchi kwenye mashindano ya Olympic ya mwaka 2020 kwa wachezaji waliochini ya miaka 23.

Aidha Mhe. Mwakyembe ameahidi kuwa serikali itaendela kuboresha mazingira ya soka nchini ikiwemo kuboresha miundombinu ya michezo huku ikiheshimu uhuru wa vyama vya michezo kwenye masuala ya kiufundi.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Bw. Musa Chaulo amewataka wajumbe wa kamati kuu ya TFF kuwatendea haki watanzania kwa kuchagua viongozi wanaostahili na watakaoweza kuwaletea wapenzi wa soka nchini raha badala ya karaha.

Bw. Chaulo amesema kuwa uwajibikaji na utendaji unaozingatia haki ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo ya soka kuanzia timu ama vilabu  vidogovidogo na timu ama vilabu vikubwa vinavyoiwakilisha nchi katika michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Naye mwakilishi kutoka FIFA Bw. Solomon Mudege amewahasa wagombea kuwa yeyote anayetaka kugombea uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TTF) kwa lengo la kujipatia fedha amepotea njia na hana sifa ya kuwa mgombea kwani uongozi ni dhamana inayomtaka mtu kusimamia kwa dhati na kuendeleza michezo ndani na nje ya nchi.

About bukuku

Check Also

IMG_0024-750x350

SEKRETARIETI YA TFF YAWASHTAKI WANNE KWENYE KAMATI YA MAADILI

  Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × 1 =