Saturday , November 17 2018

Home / MCHANGANYIKO / MSTAHIKI MEYA WA KINONDONI SITTA ASEMA BILIONI 4.5 ZIMETENGWA KWA AJILI YA MIKOPO KWA WANAWAKE NA VIJANA

MSTAHIKI MEYA WA KINONDONI SITTA ASEMA BILIONI 4.5 ZIMETENGWA KWA AJILI YA MIKOPO KWA WANAWAKE NA VIJANA

NA MWANDISHI WETU

 

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Benjamin Sitta amesema sh. bilioni 4.5 zimetengwa kwa ajili ya mikopo kwa wanawake na vijana.

 

Fedha hizo zitatumika kwa miaka mitatu ambapo kwa kunzia sh. bilioni 1.5 zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

 

Kwa mujibu wa Meya Sitta, fedha hizo ni swa na asilimia 10 ya mapato yatokanayo na makusanyo ya ndani kwa mwaka ikiwa ni utekelezaji wa sera inayozitaka halmshauri  na manispaa zote nchini kutenga mifuko maalumu kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi wanawake na vijana.

 

Meya Sitta alisema hayo alipozungumza na wakazi wa Kawe kwenye viwanja vya Tanganyika Packers kuzungumzia kero za huduma mbalimbali  za jamii.

 

Alitoa wito kwa makundi yenye sifa kuchangamkia fursa ya fedha hizo na kuzifanyiakazi kadri itakavyoelekezwa ili kujikwamua kiuchumi wakati wa utekelezaji wa mradi yao.

 

Alisema halmashauri hiyo imeanza kuboresha miundombinu ya maji, umeme, vyoo, barabara na vibanda vya kisasa ili kuwa na mazingira bora ya kufanyia biashara kwa wajasiriamali wadogo katika maeneo iliyotenga kwa ajili yao.

 

Meya Sitta aliwaambia wakazi hao kuwa, halmashauri hiyo imeanza kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kwa ajili ya kujenga stendi ya kisasa ya mabasi ya daladala Kawe na maeneo ya wafanyabiashara wadogo.

 

“Wafanyabiashara wote walio katika maeneo yasiyo rasmi kwa biashara na hatarishi watatambuliwa na kuwezeshwa kupitia mpango maalumu wa mfuko wa kuwawezesha wanawake na vijana unaosimamiwa na manispaa yetu,” alisema Meya sitta ambaye pia ni Diwani wa Msasani.

 

Hivi karibuni Rais John Magufuli aliwaagiza viongozi wa halmashauri, Manispaa, Miji, Mikoa na Wilaya zote nchini kutenga maeneo rafiki na yanayofikika kwa wafanyabiashara wadogo.

About Alex

Check Also

IMG_5910

MAZOEZI YA PAMOJA YA MAJESHI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAMEWAPA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA MBALIMBALI

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akizungumza wakati akifunga kufunga …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × five =