Saturday , November 17 2018

Home / MICHEZO / SAMATTA ATUPIA MAWILI KRC GENK IKIISHINDILIA 5-3 ANTWERP MCHEZO WA LIGI KUU UBELGIJI

SAMATTA ATUPIA MAWILI KRC GENK IKIISHINDILIA 5-3 ANTWERP MCHEZO WA LIGI KUU UBELGIJI

mbwana-samatta-europa-genk-09032017_1i8svjjcmytoi1xlzy23y3lcpo

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania ameendelea kung’ara nchini Ubelgiji, baada ya leo kufunga  mabao mawili na kuseti mawili, timu yake, KRC Genk ikishinda 5-3 dhidi ya wenyeji, Royal Antwerp FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchini humo, Uwanja wa Bosuilstadion, Deurne.
Samatta alifunga bao la kwanza dakika nane na la nne dakika ya 41 na akaseti la pili lililofungwa na mshambuliaji Mbelgiji, Leandro Trossard dakika ya 16 na tano ambalo beki Mbelgiji, Dino Arslanagic alijifunga dakika ya 59 wakati bao la tatu la Genk limefungwa na mshambuliaji Mbelgiji, Siebe Schrijvers dakika ya 21.

Mabao ya Antwerp yamefungwa na kiungo Mbelgiji,  Joeri Dequevy dakika ya 24, mshambuliaji Mghana, William Owusu Acheampong dakika ya 79 na Arslanagic dakika ya 81.

About Alex

Check Also

images

RT yamtambulisha mkufunzi kutoka Japan

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), jana limemtambulisha Mkufunzi wa kujitolea kutoka nchini Japan, Ayane Sato. …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × one =