Saturday , November 17 2018

Home / MICHEZO / SIMBA YAITANDIKA MTIBWA SUGAR YA MANUNGU GOLI 1-0, EMMANUEL OKWI AFANYA KWELI

SIMBA YAITANDIKA MTIBWA SUGAR YA MANUNGU GOLI 1-0, EMMANUEL OKWI AFANYA KWELI

1

Wachezaji wa timu ya Simba ya Dar es salaam na Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro wakiingia uwanjani kwa ajili ya mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam  jioni ya Leo, Ikiwa ni mchezo wa majaribio kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi Kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Katika mchezo huo Simba imeibuka Kidedea kwa ushindi wa goli moja dhidi ya Mtibwa Sugar  ambalo lilifungwa na Mshambuliaji Emmanuel Okwi. washambuliaji wa timu ya Simba walikosa magoli mengi katika lango la Mtibwa Sugar.

Kocha Joseph Omog anahitajika kurekebisha kasoro ndogondogo zinazotokana na ubutu wa safu ya ushambuliaji ya timu ya Simba kwa ni mchezaji Haruna Niyonzima amefanya kazi kubwa kuunganisha mipira kwa washabuliaji wa timu hiyo lakini washambuliaji John Bocco, Emmanuel Okwi Shiza Kichuya ama walikosa magoli kwa kupiga pembeni ama waliachiana mpira ukakosa mpigaji na wakati mwingine Mlinda mlango wa Matibwa Sugar alizuia mipira hiyo kuingia golini.

2

Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

3

Kikosi cha timu ya Simba kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo huo.

4

Mshambuliaji wa Simba John Bocco akichuana vikali kuwania mpira dhidi ya mchezaji wa Mtibwa Sugar wakati mchezo huo ukiendelea.

5

Mshabuliaji wa timu ya Simba Shiza Kichuya akiwania mpira na beki wa timu ya Mtibwa Sugar.

6 7

Golikipa wa timu ya Mtibwa Sugar Shaban Kado akitolewa nje ya uwanja mara baada ya kuumia katika mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Simba na Mtibwa Sugar.

8

Mshambuliaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi kulia akishangilia pamoja na wachezaji wenzake mara baada ya kuifungia timu yake goli kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro.

About bukuku

Check Also

images

RT yamtambulisha mkufunzi kutoka Japan

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), jana limemtambulisha Mkufunzi wa kujitolea kutoka nchini Japan, Ayane Sato. …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twenty − two =