Monday , October 15 2018

Home / MCHANGANYIKO / WILAYA YA KISHAPU YAZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA KILIMO NA ELIMU

WILAYA YA KISHAPU YAZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA KILIMO NA ELIMU

1

Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha shughuli za kilimo na elimu kwa wananchi.

2

Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Godwin Everygist akifafanua jambo kwa wananchi wakati wa uhamasishaji wa shughuli za kilimo.

3

Ofisa Elimu Sekondari halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Cleophas akihamasisha wananchi kushiriki shughuli za elimu.

4

Ofisa Elimu Msingi halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Moshi Balele akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji elimu na kilimo kwa wananchi.

5

Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi wilayani Kishapu.

…………………….

Na Mwandishi Maalumu, Kishapu

Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imezindua kampeni kabambe ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za kilimo na elimu.

Imezindua kampeni hiyo katika kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi ambayo itashirikisha wananchi katika vijiji vyote vya wilaya hiyo ili kuinua hali za wananchi kiuchumi na kielimu.

Akizindua kampeni hiyo wa niaba ya Mkuu wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba, Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese alisema kila mwananchi ana wajibu wa kutumia fursa ya ardhi kujiletea maendeleo.

Kengese alimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili hali ya ukame kutokana na hali ya hewa ya wilaya hiyo ambayo hupata mvua chini ya wastani unaotakiwa.

Alisema halmashauri ya wilaya hiyo kwa kutambua hali ya hewa ilitunga sheria ndogo mwaka 2008 ya kilimo cha mazao yanayostahimili ukame na hifadhi ya chakula cha kutosha kwa kaya.

“Sheria hii imemtaka kila mkazi wa wilaya ya Kishapu kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwa ni pamoja na kuhifadhi chakula cha kutosheleza mahitaji ya familia angalau miaka miwili au zaidi.

“Aidha sheria hii ilitungwa ili kutuhakikishia usalama wa chakula muda wote hivyo ni rai yangu kuwa wananchi wote tutashiriki katika shughuli za kilimo kwa kulima mazao yanayostahimili ukame,” alisisitiza.

Aidha, Kengese aliongeza kuwa sheria imetaja adhabu kwa mtu atakayekadi adhabu yake ni kifungo kisichozi miezi 12 au kulipa faini isiyozidi sh. laki tatu au adhabu zote mbili.

Pia aliwataka maofisa kilimo waisimamie sheria hiyo kikamilifu na kuwa yeyote atakayekaidi afikishwe kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

 

About Alex

Check Also

3K

TFS YAHAMASISHA UTALII WA KIIKOLOJIA KWA WATANZANIA

Afisa Misitu Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS),Arijanso Mlog akizungumza na Waandishi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 − twelve =