Thursday , January 17 2019

Home / BIASHARA / Makamu wa Rais Ahudhuria Kilele cha Miaka 50 ya NBC

Makamu wa Rais Ahudhuria Kilele cha Miaka 50 ya NBC

15

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya benki ya NBC iliyofanyika jana usiku kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

6

  Msanii Mkongwe na Maarufu  kutoka Afrika ya Kusini Yvonne ChakaChaka akitumbuiza kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya benki ya NBC iliyofanyika jana usiku kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)31

Mwenyekiti wa Bodi ya NBC Ndugu Nehemia Mchechu akihutubia katika hafla ya kilele cha maadhimisho  ya miaka 50 ya benki ya NBC iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

11

Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya benki ya NBC iliyofanyika jana jijini Dar es salaam.

…………………………………………………………………………………..

Mwenyekiti wa Bodi ya NBC Ndugu Nehemia Mchechu akihutubia katika hafla ya kilele cha maadhimisho  ya miaka 50 ya benki ya NBC iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Bodi na Menejimenti ya NBC na Mabenki mengine kuwa kuanzia sasa Taasisi zote za fedha ziweke kipaumbele cha kwanza katika kuwezesha kuendeleza viwanda nchini hasa viwanda vidogo vidogo na vya kati vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.Pia viwanda ambavyo vinatumia teknolojia ya kati na nguvu kazi zaidi ( labour intensive technology).

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akihutubua kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya NBC.

Mhe. Samia alisema mabenki mengi yameendelea kutoza riba ubwa hivyo kupelekea wananchi wa kipato cha chini hivyo aliwataka Wataalamu wa NBC na Sekta za Fedha kwa ujumla kutafuta suluhisho la riba zisizo rafiki kwa walio wengi ili amana pamoja na mikopo iweze kuongezeka.

Makamu wa Rais aliziagiza Bodi na Menejimeni ya NBC na Mabenki yote nchini kuzingatia Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha, alisema ” Serikali ya Tanzania haitomuonea mtu haya na itachukua hatua kali dhidi ya benki au Taasisi yeyote itakayobainika kukiuka matakwa ya sheria hiyo.”

Mwisho Makamu wa Rais aliipongeza benki ya NBC kwa kuweza kutoa gawio la Shilingi Bikioni 1.2 mwaka huu 2017 kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.

About Alex

Check Also

1R6A0323

MHE HASUNGA ASHUHUDIA HAFLA YA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UBANGUAJI KOROSHO

  Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania Dkt Hussein Mansoor (Kushoto) akisalimiana …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − 9 =