Wednesday , January 16 2019

Home / MICHEZO / OKWI NNE,SIMBA YAIDUNGUA WIKI RUVU SHOOTING SHAMBA LA BIBI VPL

OKWI NNE,SIMBA YAIDUNGUA WIKI RUVU SHOOTING SHAMBA LA BIBI VPL

 

ok1

Mshabuliaji wa timu ya Simba Emmanuel Arnold Okwi akimtoka mchezaji wa timu ya JKT Ruvu wakati timu hizo zilipofungua Dimba la Ligi Kuu ya Vodacom 2017/2018 kwenye uwanja wa Uhuru  huku timu hiyo ikiibuka na ushindi wa Magoli Saba Emmanuel Okwi akifunga magoli manne peke yake.

ok2

Mshabuliaji wa timu ya Simba Emmanuel Arnold Okwiakiwaongoza wachezaji wenzake kushangilia goli la Nnne aliloifungia timu yake ya Simba katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru .

ok3

Kikosi cha timu ya JKT Ruvu kikiwa katika picha ya pamoja.

ok4

Kikosi cha timu ya Simba kikiwa katika picha ya pamoja.

……………………………………………………………………………………………….

Mabingwa wa Kombe la Ngao ya Jamii timu ya Simba  imeanza vema Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kupiga wiki yaani magoli 7-0 Ruvu Shooting ya Mkoani Pwani mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru ‘Shamba la bibi’ jijini Dar es salaam.
Mshambuliaji wa Zamani wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Emmanuel Arnold Okwi ameonesha kuwa  Simba haikufanya makosa kumrejesha baada ya kufunga goli nne peke yake akimjibu Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe alipofanya hivyo Mwaka 2015 alipoifunga timu ya Coastal Union ya Tanga mabao manne kwa ushindi wa jumla  ya mabao ya 8-0 ikiwa chini ya Jamhuri Kihwelu ‘Julio’.

Okwi alifungua sherehe za mabao dakika ya 18 akimchambua kipa Bidii Hussein baada ya pasi ya Muzamil Yassin na bao la pili akafunga dakika ya 22 baada ya kuwachambua mabeki ndani ya boksi kufuatia pasi ya kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.
Okwi akakamilisha hat trick yake dakika ya 35 baada ya pasi nzuri ya Muzamil tena kabla ya kusaidia kupatikana kwa bao la nne.
Okwi aliwatoka wachezaji wa Ruvu Shoting hadi karibu na boksi na kumpasia beki Erasto Nyoni pembeni kushoto, aliyetia krosi iliyosindikizwa nyavuni na winga machachari, Shiza Kichuya kuipatia Simba bao la nne dakika ya 42.
Mshambuliaji wa zamani wa Zesco United ya Zambia, Juma Luizio Ndanda akaifungia Simba bao la tano dakika ya 44 akimalizia krosi ya Nyoni, kabla ya Okwi kufunga bao lake la nne leo na la sita katika mchezo dakika ya 52 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo Saidi Hamisi Ndemla.
Beki aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC baada ya kusajiliwa kutoka Azam FC, Erasto Edward Nyoni akakamilisha shangwe za mabao za Wekundu wa Msimbazi kwa kufunga la saba dakika ya 81.
Katika mechi nyingine za Ligi Kuu leo; bao pekee la mshambuliaji Mghana, Yahya Mohammed limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Mwadui imeshinda 2-1 dhidi ya Singida United Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Mtibwa Sugar wameilaza 1-0 Stand United Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Mbao FC wameshinda ugenini 1-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Tanzania Prisons nayo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mji Njombe na Mbeya City imeilaza Maji Maji ya Songea 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. 
Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo kati ya mabingwa watetezi, Yanga SC kuikaribisha Lipuli ya Iringa Uwanja wa Uhuru.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Ally Shomary, Erasto Nyoni, Method Mwanjali/Juuko Murshid dk65, Salim Mbonde, James Kotei, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin/Said Ndemla dk46, Juma Luizio, Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk43.
Ruvu Shooting; Bidii Abdallah, Said Madega/Amani George dk50, Yussuf Ngunya, Shaibu Nayopa, Mangasini Mbonosi, Baraka Mtui, Chande Magoja, Shaaban Msala, Ishara Said, Jamal Mtegeta na Khamis Mcha ‘Vialli’/Said Dilunga dk46.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Ally Shomary, Erasto Nyoni, Method Mwanjali/Juuko Murshid dk65, Salim Mbonde, James Kotei, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin/Said Ndemla dk46, Juma Luizio, Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk43.

 

About Alex

Check Also

IMG_5775

Wananchi kata ya Kala Wamlilia RC Baada ya kukosa Mawasiliano ya Simu Una Radio

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akiongea na wananchi wa Kijiji cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × 2 =