Wednesday , October 17 2018

Home / BIASHARA / NIC Bank Yakabidhi Magari Matatu kati ya Sita Kwa Mteja wake kama Mkopo

NIC Bank Yakabidhi Magari Matatu kati ya Sita Kwa Mteja wake kama Mkopo

Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro(kulia) akizungumza jambo na mmoja wa wateja waliofika kwaajili ya kukabidhiwa magari makubwa ikiwa awamu ya kwanza ya mkopo wa Magari Sita ambapo leo amepokea magari matatu na matela matatu
Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro(kulia) akimkabidhi funguo  Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw.Zainul Dossa(kushoto) za magari matatu waliyokopeshwa na Benki ya NIC
Meneja Uendeshaji kutoka Kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw. Arif akiwasha moja ya gari mara baada ya Benki ya NIC kukopesha magari sita kwenye kampuni ya Usafirishaji ya Simera leo jijini Dar es Salaam.
Magari matatu kati ya sita yalikabidhiwa na benki ya NIC kama mkopo kwa mteja wao

Leo benki ya NIC imekabidhi magari makubwa matatu na matela yake kati ya magari sita ambayo yamekabidhiwa kama mkopo kwa Mteja wao Simera. Makabidhiano ya Magari hayo yamefanyika katika Ofisi za FAW zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw.Zainul Dossa amepokea magari hayo kati ya sita waliyokopeshwa na Benki ya NIC mapema leo huku magari mengine matatu yatakabidhiwa hivi karibuni.

About Alex

Check Also

IMG_0983

HALOTEL TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA MITATU YA HUDUMA TANGU IANZISHWE HAPA NCHINI TANZANIA

Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Van Son, akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 + 6 =