Wednesday , October 17 2018

Home / MICHEZO / PSG KUKAMILISHA USAJILI WA MBAPPE KUTOKA MONACO HII LEO

PSG KUKAMILISHA USAJILI WA MBAPPE KUTOKA MONACO HII LEO

Kylian Mbappe of Monaco during the UEFA Champions League Semi Final first leg match between AS Monaco v Juventus at Stade Louis II on May 3, 2017 in Monaco, Monaco. (Photo by Matteo Ciambelli/NurPhoto via Getty Images)

Mshambuliaji wa Klabu ya Fc Monaco, Kylian Mbappe anatarajiwa kukamilisha usajili wake wa mkopo na klabu ya Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG).

Mchezaji huyo anatarajiwa kutua nchini Ufaransa siku ya Leo, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Ufaransa.

Kituo cha redio cha Ufaransa siku ya Jumapili kiliripoti kuwa PSG wamekubali kulipa euro milioni 180 ambazo sawa na dola za marekani 215,000,000) ikiwa ni pamoja na mafao kwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 18.

Usajili huo utaweka historia katika uhamisho kuwa usajili wa pili wa gharama kubwa zaidi katika soka baada ya Neymar, ambaye alijiunga na PSG kutoka Barcelona kwa euro milioni 222 mapema mwezi huu.

Hata hivyo kuna wasiwasi zaidi kuhusiana na kile kilicho juu ya mkutano wa UEFA wa Fedha unaohusu gharama kubwa katika usajili wa wachezaji Fair Play (FFP) na ndio maana PSG wanataka kwanza kumsajili kwa mkopo Mbappe .

Monaco na PSG siku ya Jumapili zilifikia makubaliano ya Kylian Mbappe kwenda PSG kwa gharama ya usajili wa euro milioni 180.

About Alex

Check Also

TAIFA

TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI YA KWENDA AFCON 2019,YAIDUNGUA 2-0 CAPE VERDE

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM TANZANIA imefufua matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 − six =