Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / Taasisi ya Women On Wheel – Africa yatoa mafunzo ya udereva wa kibiashara kwa wanawake

Taasisi ya Women On Wheel – Africa yatoa mafunzo ya udereva wa kibiashara kwa wanawake

AF1

Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel – Africa akizungumza na wanawake akina mama kwa wasichana  wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya udereva wa kibiashara  ambao utawawezesha  kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

Bw. Martin Gabone amesema Semina hii ina lengo la kuwaandaa wanawake watanzania na Afrika kwa ujumla kupata ujuzi katika  taaluma ya udereva wa kibiashara ambapo wanawake hawa watapata mafunzo maalum katika programu ya Women On Wheel – Africa  ili kujiwezesha na kujitegemea kiuchumi kupitia taaluma hii ya udereva  wa kibiashara na wenye tija kwa maisha yao na taifa kwa ujumla wake.

Women On Wheel – Africa inawakaribisha wanawake akina mama kwa wasichana kujisajiri ili  kujiunga na mpango huu muhimu ambapo mafunzo yanatarajiwa kuanza mwezi wa tisa mwaka huu 2017  jijini Dar es salaam katika ofisi za taasisi ya

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutumia namba hizi
OFISI ZA TAASISI HIYO ZIPO  KINONDONI ADA ESTATE KARIBU NA  BAKWATA HIGH SCHOOL

AF2 AF3

Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ofisi za Women On Wheel – Africa Kinondoni.

AF4

Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ofisi za Women On Wheel – Africa Kinondoni.

AF5

Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel – Africa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanawake akina mama kwa wasichana  wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

AF6 AF7

Mjasiriamali Bi Tedy Daniel mmoja wa washiriki wa semina hiyo akifafanua jambo kwa wanasemina wenzake wakati wa mafunzo hayo.

AF8

Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel – Africa akiwaelekeza jambo baadhi ya  washiriki   wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

About bukuku

Check Also

MKUU WA WILAYA YA BABATI

MAHAFALI YA 41 SHULE YA SEKONDARI SINGE HAIJAWAHI KUTOKEA

Na John Walter-Babati Mkuu wa wilaya ya Babati  Elizabeth Kitundu,  amewataka wahitimu wa kidato cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

14 + eight =