Tuesday , November 21 2017

Home / MCHANGANYIKO / MWENYEKITI WA KAMATI YA MAUDHUI YA TCRA MRS VALERIE NDENEINGO AZUNGUMZA NA WAMILIKI WA RADIO NA TELEVISION ZA MTANDAONI ( ONLINE RADIO NA TELEVISION) JIJINI DAR

MWENYEKITI WA KAMATI YA MAUDHUI YA TCRA MRS VALERIE NDENEINGO AZUNGUMZA NA WAMILIKI WA RADIO NA TELEVISION ZA MTANDAONI ( ONLINE RADIO NA TELEVISION) JIJINI DAR

DSC01197

Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mrs Valerie Ndeneingo  akiongea na wamiliki wa Radio na
Television za Mtandaoni (On line Radio and Television) kwenye Ofisi ya
Mamlaka ya Mawasiliano, jijini Dar Es Salaam    tarehe 13, September 2017

DSC01201

Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano huo.

DSC01204

Baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii.

………………………………………………………………………

Awali ya yote naomba nianze kwa Kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutupa uzima nakutuwezesha kukutana kwenye mkutano huu muhimu unaozungumzia masuala ya Mawasiliano na huduma zinazotolewa na vyombo vyetu vya habari.

Nichukue  fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito na mchango wenu mkubwa mnaoutoa kupitia vyombo vyenu mbalimbali vya Mawasiliano kama vile online Radio, online televisheni, blogs na vinginevyo.Vyombo hivi ni matokeo ya ukuaji wa kasi wa teknolojia ya habari, na ni fursa nzuri kwa wanahabari kutoa na kusambaza habari mbalimbali zinazohusu jamii inayotuzunguka.

Ni miaka takribani mitano tuiliyopita, kulikuwa hakuna fursa hizi za kupata matangazo ya televisheni kupitia kwenye mitandao, na kama ilikuwepo, ubora wa picha ulikuwa hafifu. Lakini sasa huduma hii imeenea kwa watanzania wengi, na hivyo kuwepo na umuhimu wa kuisimamia huduma hii ipasavyo ili iweze kuleta tija kwenye taifa na si vinginevyo.

Mchango wenu kupitia huduma hizo sio tu unaelimisha watumiaji bali pia unatoa mwanga na fursa mbalimbali ambazo watanzania wanaweza kuzitumia kujiimarisha kiuchumi .

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kupitia Kamati yake ya Maudhui inatambua na kuthamini sana kuwepo kwa fursa hii ya upashanaji wa habari. Na ni kwa kuzingatia umuhimu huo Serikali iliamua kuruhusu huduma kama vile online Radio, online televisheni na blogs ziendelee kutolewa wakati miongozo na taratibu stahiki zikikamilishwa.

Mkutano wetu wa leo, umelenga kuzungumzia namna bora ya upashanaji wa habari na utangazaji wa matukio mbalimbali yanayotokea ,(current affairs)kupitia “vyombo vya habari mtandaoni” (On line media).

Kama mnavyofahamu, TCRA, pamoja na mambo mengine, imepewa dhamana ya kisheria kusimamia maudhui katika vyombo vya Utangazaji na vile vya ki-elekroniki. Jukumu hili, linaifanyaTCRA kuhakikisha kuwa inakuwa karibu na watoa huduma na watumiaji wa vyombo hivi nakujiridhisha kuwa vyombo hivi vinatumika kwa namna bora iliyokusudiwa katika jamii.Niendelee kusema tu kuwa TCRA inatambua umuhimu wa vyombo vya habari kupitia mitandao (online media) ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii katika kuboresha maisha ya watanzania na kuleta maendeleo.

Ni  kwa ajili hiyo, leo tumeona ni vyema kukutana na wadau wa habari kupitia mitandao na wengineo,ili tuweze kupeleka na kufikisha ujumbe kwa watumiaji wa huduma za mitandao kwa mustakabali wa nchi yetu, Amani ya nchi yetu na mafanikio ya kila mtu, mmoja mmoja, na ya nchi kwa ujumla kwamba yako mikononi mwenu.

Ni wajibu wetu kufahamu kuwa, si kila  habari tunayoipata kutoka kwa jamii inafaa kusambazwa kwa jamii. Maadili ya Uandishi tunayotumia na kuzingatia kwenye vyombo vya Utangazaji wa Radio na Televisheni yanapaswa kutumika kwenye usambazaji wa habari kupitia mitandao. Tuelewe kuwa kuna habari zingine hazina tija kwa jamii, na zingine huleta uchochezi.Ni wajibu wetu kama wadau na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhakikisha kuwa tunahabarisha huku tukizingatia kuwa habari zetu zinajenga umoja wa kitaifa, mshikamano na ushirikiano baina ya watanzania bila kujenga hofu, kuchochea chuki na uhasama baina ya watanzania.

Ieleweke kuwa kutumia   mitandao ya kijamii kutoa habari hakuondoi umuhimu wa kufuata maadili ya uandishi na upashanaji wa habari.

Maadiliya Uandishi yanatutaka kujali heshima na utu wa kila mtanzania. Mambo ya ndani ya mtu binafsi na yaki-familia, hayapaswi kusambazwa kwenye vyombo vya habari vya mitandaoni. Hii inaondoa heshima na Utu wa mtu. Habari yoyote ya mtu binafsi haipaswi kutangazwa isipokuwa pale ambapo italazimika kwa maslahi ya umma mambo hayo yatangazwe na vyombo husika.

Vyombo vya Habari kupitia mitandao vimekuwa mstari wa mbele kupotosha lugha yetu ya Kiswahili, na vilevile kutumia lugha chafu zisizo na staha kwa jamii. Tukumbuke kuwa, habari na matumizi ya lugha chafu mtandaoni kwa sasa yanasambaa kwa kasi kubwa, ikizingatiwa kuwa watumiaji wa mitandao wanaongezeka siku hadi siku. Hii ni kwa sababu matukio mengi yanapotokea, huwafikia wananchi mapema zaidi.

Ni vyema tukawa makini katika kuchagua maneno na kuwa na matumizi sahihi ya lugha kwa ajili ya kuwahabarisha wananchi wetu maana matumizi ya lugha chafu hayatavumiliwa hata   kidogo.

Tunashuhudia kuwaTeknolojia ya Habari mtandaoni, imetoa fursa kwa mtu yeyote kuwa chanzo cha habari. Kwa mfano;baadhi ya watumiaji wa mitandao wamekuwa vyanzo vya Habari, kwa kutengeneza habari wenyewe, kwa kujirekodi(clips) na kusambaza mitandaoni habari(clips) hizo. Wengine wamekuwa wakipiga picha na kurekodi matukio mbalimbali na baadaye kuyasambaza mitandaoni.

Kuwa chanzo cha habari na kusamabaza matukio ni jambo ambalo linatakiwa lifanywe kwa tahadhari kubwa. Ikumbukwe kuwa maadili ya uandishi wa Habari hayaruhusu kusambaza picha kama zile zitokanazo na matukio ya ajali zikionyesha utupu wa mtu aliyepata ajali na damu ambapo huleta hofu kwa jamii.

Amewakuwakumbusha na kuwatahadharisha kuwa ni kosa la jinai kwa chanzo chochote cha habari na usambazaji wa habari za matukio iwapo maudhui yake ni yaleyasiyofaa.

Amewashukuru sana kwa kufika kwenye kikao hiki na nitoe wito kwa kuwataka wale wote ambao wanadhamana ya kuhabarisha au kuwa chanzo cha habari na kusambaza,kuitumia dhamana hiyo huku wakijua kuwa wanawajibika kuulinda usalama wa nchi yetu.

 

About Alex

Check Also

1

TANZANIA YAPIGWA MSASA NA ISRAEL WA KUTANGAZA UTALII KIDIGITALI

Dr. Noam Koriat akitoa mafunzo kwa watumishi wa Wizara ya Utalii na Taasisi zake katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

20 + 10 =