Tuesday , November 21 2017

Home / MCHANGANYIKO / SERIKALI YAFUTA UMILIKI WA SHAMBA LA MANJI, AMBALO WALIPEWA YANGA KUJENGA UWANJA

SERIKALI YAFUTA UMILIKI WA SHAMBA LA MANJI, AMBALO WALIPEWA YANGA KUJENGA UWANJA

 Serikali imefuta umiliki wa shamba lililokuwa linamilikiwa na Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Yusuf Manji.

Shamba hilo lilili Kigamboni lenye ukubwa wa ekari 715, limerejeshwa serikalini baada ya uamuzi wa Rais John Magufuli.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema leo Jumatano kuwa, shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.

Lukuvi amesema shamba lingine la Kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa eka 5,400 pia limefutwa. Waziri amesema mashamba hayo sasa yako mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.

Lukuvi amewaonya wananchi wasivamie maeneo hayo kwa kuwa watakaokamatwa  watashitakiwa. “Muyaache maeneo hayo kama yalivyo mkijenga tutakuja kuvunja,” amesema.

Wakati hilo linatokea, Yanga watalikumbuka shamba hilo kwa kuwa Manji alijitolewa kuwa sehemu ya kujenga uwanja wa mazoezi.
Lakini tayari alikuwa na mpango wa kujenga uwanja wa kisasa kwa ajili ya klabu hiyo hasa kama wangeingia ule mkataba wa kukodisha kwa miaka 10 na kampuni yake ya Yanga Yetu Ltd.

About Alex

Check Also

1

TANZANIA YAPIGWA MSASA NA ISRAEL WA KUTANGAZA UTALII KIDIGITALI

Dr. Noam Koriat akitoa mafunzo kwa watumishi wa Wizara ya Utalii na Taasisi zake katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

20 − 10 =